MISTARI YA WIMBO HUU

Mateso yamezidi offside mitaa, haina filimbi
Mahakama iko chini ya jaji, mtuhumiwa hapati ushindi
Haki ya maskini imefichwa kwenye soksi ya tajiri
Na pesa pesa hazina pini, hujifungi mtoto wa batili
Watoto wanatelekezwa matatizo yanapobidi
Ukimwi unateketeza vijana, babu na bibi
Mziki pia hauna ofisi, vijana wanaikana shule
Waki-hit unawafilisi, huku future inaenda kule
Ah ndoto za yatima usiku zinashika tama
Pesa kwao zinapo gima hukumbuka baba na mama
Mapenzi na pesa, ni swali lisilojibika
Watoto wa shule zinapowatesa, wanapotongozwa na watu wa rika
Kauzibe, alizaliwa kijijini bila dokta
Leo hii anahukumiwa kwa kuunga wa mama Nota
Anayetuma hii salamu kwa mola atoe miujiza
Mwanga bado una damu, huku dunia imejaa giza
Ah

Mateso yamezidi mpaka najihisi sina haki duniani
Kila panapokucha afadhali tu ya jana
Mradi siku inakwenda
Tunashukuru kwa Maulana ah

Yeah
Bado vijiji vina mafua na lesso ndo ziko mijini
Wanalima tunanunua, bado wanakufa masikini
Miundo haina barabara, na mbinu hazijawekwa lami
Na wale wanaofanyiwa tohara, kwa visu vya kubania ***
Wanaobakwa na watoto wa vigogo, hawafikishwi kortini
Shehe ana imani ndogo, muumini vipi amuamini
Labor hapaheshimiki wakati amezaliwa raisi
Mafataki hawahesabiki kwenye shindano la ma-miss
Na njaa au ufukara, ndani bahari ya dhiki
Asiyenacho hathaminiki, tunaishi kama maiti
Pata picha kumekucha asubuhi na mapema
Jua limechomoza kwenye giza mfano hakuna
Watu wanahangaika wamekosa cha kutafuna
Mi naimba kwa hisia ’cause roho inaniuma
Tujikusanye kwa pamoja tuimbe wimbo wa taifa

Mateso yamezidi mpaka najihisi sina haki duniani
Kila panapokucha afadhali tu ya jana
Mradi siku inakwenda
Tunashukuru kwa Maulana ah

Siku zinakwenda, ila usikate tamaa mmh
Usilie mama
Usilie baba
Usilie wewe wewe, wewe wewe

Mateso yamezidi mpaka najihisi sina haki duniani
Kila panapokucha afadhali tu ya jana
Mradi siku inakwenda
Tunashukuru kwa Maulana ah

Mateso yamezidi mpaka najihisi sina haki duniani
Kila panapokucha afadhali tu ya jana
Mradi siku inakwenda
Tunashukuru kwa Maulana ah

Katika maisha kila siku
Kuna mengi yanatokea
Ila Mungu ndo anayepanga, right
Cha msingi usikate tamaa

It’s yo boy country boy baby
Pretty girl, Linah
Ah F-Baby

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI