MISTARI YA WIMBO HUU

First time nilipenda nikajiona nimefika
Nikajua sitotendwa machozi yasingenitoka
Nikajihada nikajawa na furaha
Mwishoe kushtuka nimezimia balaa
Akaniacha ingawa alijua kabisa
Pasina penzi lake mimi sina maisha
Akaniumiza nikadhohofika
Nikakajifariji na siku zikapita
Nikakumbuka nikasema sitokuja penda tena
Baada ya miaka kupita nikajiona nishapona
Nikayasahau machungu ya nyuma
Na nikajikuta nimependa tena
Sikuamini kabisa kilichokuja tokea tena
Majonzi ya mapenzi kunibubujika tena
Kanifanya nasema sitaki kuumizwa tena tena

Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Mi nimewapatia langu pendo wakalivunja na kuacha vidonda
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Mi nimewapatia langu pendo wakalivunja na kuacha vidonda

Kila ajae hunitumia na kwenda zake
Hathamini uhitaji wa moyo wangu kwake
Mi nimekuwa wa kulia na kupona kila siku
Bora kutopenda tena
Najua ni vigumu kuishi bila penzi
Lakini bora hivyo kuliko machozi
Sijui labda mi namkosi gani mbona wengine wafurahi penzini

Yeah
We ni mrembo mwenye class nafsi ya upendo
Uko safi ila tu una kasi ya malengo
Niliahidi kuwa muwazi ila kazi mwenendo
Umegeuka fundi mjenzi una kazi kila jengo
Kama kupendwa utapendwa na wangapi?
Salamu kwako mpendwa enenda kwa sala safi
Sina mengi ya kusema kwako mpendwa wa haki
Wangu upendo wa dhati unakwenda na wakati
Niliambiwa na machizi nikawachukulia matozi
Kumbe we paka wa mpishi unajua kila msosi
Sikuwa na nia mbaya but of course
Every man in this world has desires but never for what is lost

Tamu ya mapenzi siijui mimi
Chungu na mimi maumivu moyoni
Tamu ya mapenzi siijui mimi ehee ehee
Tamu ya mapenzi siijui mimi
Chungu na mimi maumivu moyoni eeh oh ohh

Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Mi nimewapatia langu pendo wakalivunja na kuacha vidonda
Wengine mbona wanajali upendo
Wengine mbona mwaumiza tu
Mi nimewapatia langu pendo wakalivunja na kuacha vidonda

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU