MISTARI YA WIMBO HUU

Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo mawazo

Hata ukiwa na pesa lazima uwaze
Utapanga bajeti ni nini ukafanye
Ukiwa hunazo pesa ndio yazidi
Utawaza ni wapi uende ukasake
Toto lako likiwa tukutu utawaza ulichape viboko vingapi ili likome
Walimwengu nao wakiwa ni wakusakama
Utawaza ni jinsi gani uwaepuke
Hakuna binadamu asiye na mawazo
Hata vichaa nao huwa wanawaza
Kila kitu duniani lazima uwaze
Hakuna litendekalo bila ya mawazo

Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo mawazo

Hata mimi Jay Dee pia nina mawazo (sexy Lady Jide huu)
Wazo langu nataka nunua Freelander
Ila si lazima wazo langu litimie
Wengine wawaza kuiba watajirike
Wengine kuwa warembo wasifike
Mwavita anataka kuwa mwanasheria
Amina kuwa mtangazaji maarufu
Toyoyo kujenga nyumba ya kifahari
Lenee hata yeye kuishi na mzungu
Kila mtu duniani lazima uwaze
Hakuna litendekalo bila ya mawazo

Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo mawazo

Mawazo nami mi na mawazo
Haya ndio maisha yangu ya kila siku wa commercial
Yananitinga mpaka naonekana ka mjinga
Always dili zinakataa lakini haikumkinga
Nikitembea nikiongea kichwa changu chawaza
Yaani mawazo kibao yaani ni ya kusaza
Nawazo kuhusu maisha wapi ntapata pesa
Wapi zipo sasa na ni vipi ntazinasa
Mara nyingine mi nadata
Maisha yamenielemea wengine wananicheka (owh owh owh owh)
Nshasikia wengine washajitoa roho
Machoni naona giza unafuu hata siuoni
Msaada ntapata wapi kwenye shida hatujuani
Wengine wanaongea peke yao njiani
Yote kuwaza yote mawazo tu

Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo (uuh Jay Dee nina mawazo)
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo mawazo (kila mtu na mawazo)
Haijalishi ni mazuri au mabaya (uuuh uuh)
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza (uh lala lala lala lalaa)
Mawazo mawazo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI