MISTARI YA WIMBO HUU

Wewe mama wa kufikia usimdhalilishe baba
Wewe mama wa kufikia mpendezeshe baba

Kiatu kimefumuka kimefumuka fumu fumu
We mama mdogo muonee huruma baba
Unataka bambucha eh bambucha?
We mama mdogo muonee huruma baba

Kila zuri analofanya baba mama unapinga
Nitakukabidhi hati ili tuuze nyumba
Kweli ridhiki mafungu saba kwenye hii dunia
Yote ya dunia sote tunapita

We kenua he-eh (he-eh)
We kenua ho-oh (ho-oh)
We kenua we kenua
Dawa yako inachemka
We kenua he-eh (he-eh)
We kenua ho-oh (ho-oh)
We kenua we kenua
Dawa yako inachemka

Unapenda mfuko kuliko mapenzi ya ndani ya moyo
Unajifanya huoni hadi nirudi tena Bagamoyo
Unapenda mfuko kuliko mapenzi ya ndani ya moyo
Unajifanya huoni hadi nirudi tena Bagamoyo

Hai yoyo hai yoyo
Naenda Msanda mie
Hai yoyo hai yoyo
Nikavunje nazi mie
Hai yoyo hai yoyo
Naenda kwa babu mie
Hai yoyo hai yoyo
Nikavunje nazi mie

Mmh ningependa we ujue hii dunia ina mwisho
Ukipenda upende kweli usiwe unapenda mfuko
Tena ukae utambue kila mtu ana moyo na roho
Unavofanya si vizuri mtu mzima wewe

Wee baba wee baba wanao si tushaona
Wee baba wee baba mwenzako atakuua
Wee baba wee baba wanao si tushaona
Wee baba wee baba mwenzako atakuua

Bakora kama pundamilia
Nachapwa naishia kulia
Bila sababu nanyimwa chakula baba unaangalia
Mama wa kambo anapiga kama mgambo

Pili jina langu linafifia ho ho hoo
Mama ananiita Kinyoka Mdimu ho ho hoo
Pili jina langu linafifia ho ho hoo
Mama ananiita Kinyoka Mdimu wu wu wuuh
Anatamba kwa rafiki zake
Anasema ye gusa unase
Eeh yeye na kuna mengi anaongea

Umri wako anaujua anasema kafata hela
Ee baba eh wanao si tunaonewa
Umri wako anaujua anasema kafata urithi
Ee baba eh huyo mama wa kambo

Unapenda mfuko kuliko mapenzi ya ndani ya moyo
Unajifanya huoni hadi nirudi tena Bagamoyo
Unapenda mfuko kuliko mapenzi ya ndani ya moyo
Unajifanya huoni hadi nirudi tena Bagamoyo

Hai yoyo hai yoyo
Naenda Msanda mie
Hai yoyo hai yoyo
Nikavunje nazi mie
Hai yoyo hai yoyo
Naenda kwa babu mie
Hai yoyo hai yoyo
Nikavunje nazi mie

Nikapige na manyanga ili amuache baba
Mama mwenyewe majanga baiyo baiyo baiyo baiyo
Nikapige na manyanga ili amuache baba
Mama mwenyewe majanga baiyo baiyo baiyo baiyo

Unapenda mfuko
Unajifanya huoni
Unapenda mfuko
Unajifanya huoni

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI