MISTARI YA WIMBO HUU

Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa
Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

Upole wangu simanzi eeh
Kwangu kupenda maradhi iiih
Lakini kupendwaga mi nae bahati huwaga sina…
Jichoni kwangu kibanzi eeh
Ninakapenda kamanzi iih
Oh licha ya kumthamini kama shilingi tatizo hata raha sina
Ufinyu wa mboni zangu, unatazama mengi yanayonipa mateso
Ukweli hata kupenda sina raha, ona nakonda kwa mawazo
Masikini penzi langu jina, lishakatwa na kauli roho inatoka kesho
Kutwa nzima mara eeh, mara iiih
Hata najuta kupenda

Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa
Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

Nikutwa kucha maneno
Kosa si kosa maneno ilimradi tu karaha tantalila (sina raha)
Ona sina tena mipango (aah oh aah)
Kutwa nzima nnamawazo jina mh
Aah sina raha ooh mama
Tamu ya wali ni nazi eeh
Raha ya supu mandazi iiih
Raha yangu me kupendwa tu naye lakini nyota sina
Laana napata na radhi eeh nawakufuru wazazi iiih
Kwa kung’ang’ana mi kutaka kuwa nae lakini bahati sina
Masikini roho yangu (roho yanguu)
Ingelikuwa ni nguo ningempa avae
Kila kona akipita wamsifie ila lakini ni kikwazo
Masikini penzi langu
Jina lishakatwa na kauli roho inatoka kesho
Kutwa nzima mara Eeeh! Mara Iiiiii! Hata najuta kupenda

Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa
Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa
Moyo wangu, moyo wangu mama
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI