MISTARI YA WIMBO HUU

Kila mwanadamu ana upendo kwa yule ampendae
Mwingine anawaza vipi atampata yule amtakae
Sio kwamba na-act no nipo real
Japo Msodoki ni mdogo ila na uwezo wa ku-feel
Fikra zangu zinatuma nidate kwa Maunda Zoro
Najua nitaleta jealous kwa brother Banana Zoro
Sasa vipi nikiwa Penny hivi ntakuwa free
Au kama nngekuwa na Mwasiti wa THT
Ila Penny nahisi Diamond atanisumbua
Hata Mwasiti pendo langu atalivua
Kwanza long time ago nilishazimikaga na Wema
Na skendo za magazeti moyo wangu ukamtema
Nikawachukia mapaparazi nikahisi wameharibu bahati
Moyo wangu nikauweka bond kwa Chiku mwanaharakati
Ila wote tunachana hatutadumu maghettoni
Nilipozimika na Besta, Marlaw akapiga honi
Madam Ritha na Salama wakaogopa mcharuko wa BSS
Nime-move mpaka Dar, Wolper nimchane face-to-face
Ila roho inakataa inaogopa waigizaji
Macho yalishatua kwa Flora, H Baba akamhitaji

Wapo wengi natamani kuwa nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs. Superstar nani nimwite love
Mrs. Superstar nani nimwite love

Hizi hisia zangu sidhani kama nakufuru
Sidhani kama nakufuru
Akili inanituma niende sambamba na Lulu
Ila naogopa yasinitokee ya Kanumba
Nikasukumwa nikafa wengine wakang’oa mchumba
Ama Ray C nikimcheki machoni haishi
Kile kiuno bila mfupa kingenipikia mapishi
Ila ghafla nikaogopa niliposikia ana mchizi
Baada ya kuuliza ni nani kumbe mnako Lord Izzy
Navyokupa utanipa upendo wa kina
Au tutaachana njia panda kama Amini na Linah
Kwa love sitaki kukosea niwe na mrembo mwenye visa
Niwe na Thea au nimwache nidate kwa Monalisa
Nikadata na Diva, ila sauti ni soo
Ye ni mgonjwa kwa raha zangu atanifia itakua soo
Sura pesa Aunt Ezekiel young sina hela
Vanessa Mdee najua huwezi ishi kisela
Mara Jokate kichwani akanitawala mpaka basi
Nkajua hata nikisema basi hatanipa nafasi
Namuomba Mungu anipe gift special
Kama isingekua kizunguzungu basi ningekua na Recho

Wapo wengi natamani kuwa nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs. Superstar nani nimwite love
Mrs. Superstar nani nimwite love

Usiku silali usingizi hautokei
Namuwaza Johari ila ule ukaribu na Ray
Unanipa wasiwasi na mimi sitaki nijute
Basi nikaamia kwa Dyna baada ya kusema nimvute
Shilole naogopa kumwambia yanayonisibu
Kwa khadija nikakope kopa nije kumpa taratibu
Nahisi atanihadhibu pedeshee wa yafitina
Maana atahitaji matunzo cha ajabu mimi uwezo sina
Nampenda Uwoya mtoto wake ataniitaje
Kaka au baba, Ndikumana atanionaje
Hizi hisia zangu wala siitaji maswali
Mi napenda kuitwa babu, bi Cheka atakubali

Wapo wengi natamani kuwa nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs. Superstar nani nimwite love
Mrs. Superstar nani nimwite love

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI