MISTARI YA WIMBO HUU

Ah
Msela msela msela

Msela msela msela
Yoh
Watu tumeshadata
Na hili ghetto life style
Shad Bakren au Nelly wa X-plastaz
Hey Dark Master nitembezee chata
Kisha nipe kipaza nihubiri kama pastor
Ndani ya ghetto ni mengi yashatukuta
Lakini masela bado tunakomaa kutafuta
Bado tunazisaka hata kwenye vichaka
Atafutae hachoki akichoka ndio ameshapata
Japo sometimes kile kitu unachopata ni tofauti kabisa na kile unachotaka
Ila mwanaume lazima ujifunze kuridhika
Kwani ukichagua sana hukawii kutoka kapa
Duniani wote hatuwezi kuwa sawa
Na ndio maana wapinzani wa jadi mnapagawa
Kama nipo juu ni juu
Ningoje chini au nifate juu uvunjike guu
Masuper star tunang’aa kwa pamba tunazovaa
Zinafika njaa ila tunapokaa
Wengine nyumba ta udongo nyasi mlango wa gunia
Ndani hakuna mwiko kikombe wa sufuria
Zaidi ya kiberiti tu na kipande cha mkeka
Na nikishakula mambo yangu nauweka
Wala sioni hatari kula dona dagaa
Si kuna wengine hawajauona wamelala na njaa
Na usione tumepinda migongo ukadhani ni vibyongo
Pengine ni ufupi tu wa mlango
We endelea kula bia acha mi nikapate gongo
Mradi wote tuwe stim ndio life ya kibongo

Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama
Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama

Maisha ya kisela si sawa na usela mavi
Kunya wazi wazi kama unavyofilili mdwanzi
Acha unazi nipe nafasi niweke wazi
We unafikili usela ni kuwapora watu
Kulazimisha watu eti walale saa tatu
Hiyo tabia sijui umeipata wapi
Wakati msela kama ras
Jah Rastafari hana wasi
Usivamievamie vitu ovyo utaenda kombo
Msela mtu safi na anamoyo safi wa kiskauti
Kama Leader Nyaki au Masta Shafii

Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama
Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama

Walishaomba mechi mwanangu ili watupige
Tukishafika watutimue mazagazaga wayaibe
Eti kisa tu wanataka Muhamedi kauzibe
Aha kumbe unafikiliaga tu dezo
Iweje maneno yako mengi kuliko maelezo
Ganga mavumba buku 20 mpaka 60
KR bado nipo makini
Na nafikili ni lini tawini
Kila mtu nayemsuga ananambia bado yupo porini
Naamua kushika mpini kusonga mbele
Nasikia uchungu kuambiwa Juma Nature ni mtu wa misele
Mambo yenyewe cha mtoto acha ngedere
Cheza ucheze kama Pele
Aisee haka kakitu kabatwangwa
Uncle dili zimekushinda sasa unawanga
Leo ni leo asemaye kesho mwongo

Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama
Mimi msela kitu gani ufanye bwana
Mimi msela mpaka usawa unabana
Mimi msela hata chai inashindikana
Mimi msela naona kina kuja mlama

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU