MISTARI YA WIMBO HUU

Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka

Nimewekeza miaka kibao kwa hapa nlipo mwana
Sikuzaliwa kwenye mali ilibidi kuhangaika sana
Sio mambo safi, pua zangu zinanusa mkwanja
Hustler kama Alish Kuba, natimba kila kiwanja
I am the magnifico, piga kazi za hatari
Siogopi tena mkisema yote nshayasikia tayari
Maneno hayawezi niua yanafanya niwe ngangari
Nasema hewallah kwa kila jema na shari
Wengi mmefeli mnatamani maisha yangu
Mnatamani mngekuwa mimi, mnatamani hustle zangu
Nawaona ka ndugu zangu, nawachukulia wenzangu
Kumbe wenzangu mkikata kona mnageuka maadui zangu
Acheni uoga, sio lazima uwe na hoja
Ni-diss tu kama Inspector, dandia treni kwa mbele
Msiojua ndo mnavyotoka
Kifua changu kina mengi ambayo hamuwezi kuyabeba
Mkifahamu navyofikiri mtatamani mniite baba

Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka

Mnapenda kuwa powerful, mnapenda kuwa nyinyi juu
Mnatamani redioni zisikike sauti zenu tu
Mnatamani ramani igeuke, nyi ndo muwe jungu kuu
Mnaona kama dunia ni yenu, sisi tupo mradi tu
Sita-surrender forver, kwanza hii ndo chapter ya kwanza
Ka mnangoja nikate tamaa inabidi mniue kwanza
Hustle hazina mapumziko kwangu ni usiku na mchana
Niamini Mungu ananiona na kweli ananijalia sana

Kabla mliuliza naolewa lini
Baadae eti nitazaa lini
Na tena nitaachika lini, sijui hata mnataka nini!
Baadae mtauliza nakufa lini
Au kimuziki nitashuka lini
Anasemwa raisi Kikwete, sembuse mimi binti Machozi

Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka

Mbuzi tingisheni mikia, ufalme hauji kwa kuongea
Na (kila mnapoongea) mambo yanazidi tuendea
Mziki haunipi wanawake tu, unanipa michongo
Ulaya kama naenda Ilala hamuwezi funga milango
Hamnikoseshi usingizi, mbio zangu hamzipunguzi
Na hakuna hata kati yenu anaefika nusu ya hizi pumzi
Sina love hata kwa mbali, siigizi, kweli siwajali
Mnapinga kudra za Mungu na mna hasira juu ya ukweli

Mna majuto moyoni, mwajichekesha usoni, kwanini?
Mnashikana mikono miaka 50 ya ndoa
Mkirudi ndani mnalia, tofauti yangu na nyinyi ni ipi?
Kushindwa kuhimili maumivu leo nimekuwa topic

Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka
Msiache kuongea, ongeeni mnavyoweza
Kila mnapoongea sifa zinaongezeka

Yeah, it’s the boy
The Mafia, B
Na Komando Jide
You know I love you, girl
Hermy B, B-Hitz

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI