MISTARI YA WIMBO HUU

Msinisemee ah msinisemee ah
Msinisemee ah msinisemee ah
Kama napenda kula
Msinishangae msinishangae
Msinishangae msinishangae
Kama napenda kula
Msinitengee msinitengee
Msinitengee msinitengee
Kama napenda kula

Basi hivi juzi juzi
Kulikuwa na shughuli
Mtaa wa pili tena si mbali
Kulikuwa na pilau na wali
Basi nami nikajiunga
Pale pale kupiga mpunga
Watu wakajipanga
Nikaanza kwa tonge na nyama
Ni nyama tonge ni nyama tonge
Ni nyama tonge mpaka wakanifukuza
Nikasema sijali nikatoa pesa mfukoni
Nikanunua mayai kilichofuata watu hawakai

Msinisemee ah msinisemee ah
Msinisemee ah msinisemee ah
Kama napenda kula
Msinishangae msinishangae
Msinishangae msinishangae
Kama napenda kula
Msinitengee msinitengee
Msinitengee msinitengee
Kama napenda kula

Ilikuwa Jumapili
Siku ya watu wenye ufahari
Kujirusha sehemu mbali mbali
Nami nikasema leo sikubali
Wacha niendee wacha niendee
Wacha niendee ila pesa sina nataka nikale
Nikapita sokoni
Nikaomba embe sokoni
Nikaelekea baharini
Nikawaona wengi ufukweni
Napita na embe kiutani
Nakula ili watamani
Mate yaliwajaa midomoni
Basi wote wakaanza kuniomba
Msiniombee msiniombee
Msiniombee si mnasema mimi napenda kula

Msinisemee ah msinisemee ah
Msinisemee ah msinisemee ah
Kama napenda kula
Msinishangae msinishangae
Msinishangae msinishangae
Kama napenda kula
Msinitengee msinitengee
Msinitengee msinitengee
Kama napenda kula

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU