MISTARI YA WIMBO HUU

Hizi ni zama za wakali, kuchora mistari
Aa maisha ya habari, mwingi ka habari
Ukigusa hatari, nachoma na makali
Na bosi sio Zari, zali kuokota
Speed kali imefungwa mota
Mashine inatokota
Kazi, kazi, kazi jasho linatoka
Pachu pachu suti juu moka
Tuliobaki pale walipoondoka
Aah    Nguvu sio gesi au Coca
Nachomeka palipochomoka
Yei yei yei, uza sura, sauti piga bei
Mtoto mdogo cheza chei chei
Maseke, walete, wapembete
Wapunguze mapepe
Kisha waloweke, loweke, loweke
Hamsa-hamsa, mia
Juu tunajazia, hatutoki kwenye ile njia
We fatilia, uza karanga na cheza vanga
Kichange
Hatua moja usiache watoto watambe
Uza, uza, uza, uza, uza, uza, uza, uza, uza, uza

Uza karanga moe piga debe ee ehee
Mazaga ubebe ukanyee kidebe ee-eh hee
Zigi zaga, kuna zigi na sanda
Zipi baba, kuna ligi utasanda
Een’hee, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche
Wewe, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche

Tunaishi kama soldier na deal za kuuza scraper
Mwendo ni mlo mmoja na machizi tunanenepa
Dhiki haikwepeki, ukiwa nacho hakiombeki
Sakafu zimechakaa hazifai hata kupigwa deki
Check, chako chetu, cha kwetu chetu wenyewe
Kwetu ukijifanye chetu, unachetuka na chenyewe
Omba upewe, iba unyewe
Hiki kitaa kina wenyewe
Mkubwa ndevu, mdogo ndevu, kitaani wote mamwewe aah
Mtaa wa nyuma una mzee anauzaga gongo
Halafu mtoto wake polisi, ila fresh hakuna mchongo
Kama mzazi hajakufunza utakula ngada na ndumu
Maana mtaani kuna funza hadi duka la perfume
Kifupi mtaa wetu umelaaniwa
Hata umuite demu haji maana anaogopa kuibiwa
Kitaa hiki maseke, kitaa hiki makeke
Kutwa natembea na rungu kitaani wananiita Kipepe

Uza karanga moe piga debe ee ehee
Mazaga ubebe ukanyee kidebe ee-eh hee
Zigi zaga, kuna zigi na sanda
Zipi baba, kuna ligi utasanda
Een’hee, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche
Wewe, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche

Nakatiza kona zote za mtaa kimagumashi
Lengo nidake chapaa nimtunze baby na bi mdashi
Kichwa kimejaa akili nyingi zenye utashi
Naleta balaa aah mitaa ubaridi mi siupashi
Harakati za miguu na zaga kwenye begi
Umasikini sio wa unafuu na dili feki sizitegi
Silegi, matunda machafu kitaa simegi
Nigongee fegi, ubanda nipate pegi
Aa chachamaa mitaa siipotezi saa
Kila wasaha nawaza jinsi ntaikimbiza njaa
Sio pamba za kuvaa, kung’aa, kuonekana star
Mtaani kwetu maisha karata nazichanga hata bar
Msingi kiuno    Huku kwetu msingi mbio
Ukiremba ukidakwa, watu wanageuza machinjio
Nakwapua mtaa huu, natokea mtaa wa pili
Na nguo nishabadili
Dibo

Uza karanga moe piga debe ee ehee
Mazaga ubebe ukanyee kidebe ee-eh hee
Zigi zaga, kuna zigi na sanda
Zipi baba, kuna ligi utasanda
Een’hee, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche
Wewe, kitaa hiki maseke
Bila mafekeche, kitaa huku ni cheche

Baba, uliye juu jina utukuzwe
Ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani ama mbinguni
Utupe leo mkate wetu wa kila siku (Amen   )
Hol’ up    Baba unajua hawa uongo wa siku maana
Wanatuwinda, tunajipinda ili tuishi
Wanatuona wajinga, wasanii tumepinda hatuna ubishi
Hol’up, hol’up, hol’up… (wanatuloga lakini they can’t do it)
Okay, I’m ready
Kama umenisoma basi crack, crack okay
Ni rap, rap okay
Nipe mkwanja nikufanyie shoo chap chap, okay
Hii ni uswazi mpaka O’bay
Nawashusha kata K
Chezea mistari yangu inawapwaya every day
Who dat, who dat
Country Weezy, baby
Hii kwa ma baby mpaka sss wanangu wanao blaze
Y’already know, it’s the remix
Don, you crazy

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI