MISTARI YA WIMBO HUU

Vipi, kina kaka mtakwisha
Kina dada mtakwisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, wananchi mnakwisha
Serikali inatisha
Hili gonjwa linatisha

Tanzania kama si umasikini
Maendeleo, afya, ukimwi na maji
Fahamu haki zetu sisi binadamu
Utawala bora wala si elimu
Hebu zipi haki za mtoto?
Chama kizuri au uzazi wa mpango?
Au ada ya shule ya msingi?
Tutajua tumefanikiwa wapo

Vipi, kina kaka mtakwisha
Kina dada mtakwisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, wananchi mnakwisha
Serikali inatisha
Hili gonjwa linatisha

Yote tisa, kumi hili gonjwa
Sababisha ukimwi kweli ni noma
Wananchi wote mtakwisha
Hebu cheki tahadhari kote pita
Cheki ndugu, rafiki, wote wamekwisha

Vipi, kina kaka mtakwisha
Kina dada mtakwisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, wananchi mnakwisha
Serikali inatisha
Hili gonjwa linatisha

Ukipenda sana ngono, ukimwi utakushikisha adabu
Na hakuna daktari ataekupa matibabu
Hata watu wa sensa watakataa kukuhesabu
Sababu wanajua kesho utawaharibia hesabu
Utatamani ukipe rushwa kifo ili uendelee kuishi
Nashindwa kuelewa itakuaje siku yako ya mazishi
Watu hawataamini wanachokiona machoni mwao
Wanajua umetangulia watakaofuata watakuwa wao
Mitaa yote ya Bongo itatawaliwa na kilio
Sababu kwenye ngono ndugu ulikuwa tishio
Ole wao wanaochangia mpenzi mmoja
Sababu wajue kifo chao kitakuwa kimoja
Nyakati za usiku hawakosekani kona za giza
Wanajua wana ukimwi lakini hawaachi kuueneza
Soggy na TID tunawapa ushauri wa bure
Kuhusu miwaya, ngoma, ukimwi yaani minyenyere

Vipi, kina kaka mtakwisha
Kina dada mtakwisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, wananchi mnakwisha
Serikali inatisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, kina kaka mtakwisha
Kina dada mtakwisha
Hili gonjwa linatisha
Vipi, wananchi mnakwisha
Serikali inatisha
Hili gonjwa linatisha

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI