MISTARI YA WIMBO HUU

Hiki kizazi kimevurugwa na Hapa Kazi
Tupe dili wape dili nataka kuchapa kazi
Old school new school vibe
Wakongwe walinukisha si tunazirudisha vibe
Ni nani anaebisha si tumetisha zaidi ya babu
Tunaiendeleza hii sanaa na tuna nyingi tu ghadhabu (gadhabu)
Yes ma-underground tunafanya rap inang’ara
Media zinaboa wanavyotufanya mafala
Tumechoka ku-hustle mipauko chini ndala
Na hatujala usiku kazini nyie mmelala (nyie mmelala)
Tukopesheni promo tupige mikono
Tugonge vitu vinono ili wafunge hiyo midomo
Darasa hili somo piga mishono
Hivi vita havifundishwi darasani kama ngono
Dundo hili kali kitambo lilisumbua
Siku hizi emcee mkali eti video inatusua
Conscious emcee anasifa ya kubana pua
(Una sound sexy) Sio zangu kampe Makamua
Kuna mtu anaenijua Mi bingwa wa kuzibua
Eti Mweusi Washamba mnapanda meli ya mabua
Mnahema mkipanda mkishuka tu mnapumua
Wengi mnalindwa na irizi mi ndo nalindwa na dua
Game imejaa majipu Koli natumbua
Chunusi kausha niache mi ni-deal na surua

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Kwi kwi Ulamaa Professor Jay Afande

Game ishakuwa ya wadau
Tale ana nguvu ya kufanya media house wakudharau
Kama hauna hela kajiunge Mkubwa Fella
La sivyo utaendelea kuwaimbia masela
DJ kaku-support wiki mbili tu we unaringa
Mkikutana Leaders ye vinjwaji anazinga
We unatungua za Chidi mapenzi mwenzio ana winga
Una raba ya buku tano tena ya asante-machinga (what you say)
Siku hizi shabiki anaamuliwa (gimme a break)
Kwa kuwa bando na vocha amenunuliwa (duh)
Kina Kasanula daily wanavyosujudiwa
Niko nyumbani Davido napeta mi nabaniwa
Imetosha sasa tumebeba sana unga
Shida yetu mchele so tubebesheni mpunga
Tunawapa utajiri si tunaishia kujidunga
Na wanaoshindwa kukaza wanaishia kuwa mapu***
Ka unapata moja kwanini usipate mia
Na hii inawezekana kwa wote mlio na nia
Sioni sababu mi za kushinda kwenye mitaa
Na kama nna kipaji kwanini nife na njaa

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Kwi kwi Ulamaa Professor Jay Afande

Niko ghetto namsikiliza Nash MC “Zima”
Nikimimina juice ya mango garden na Fina
Huku natafakari kesho ya tasnia
Sa sikia ushikaji ndo mtaji na cash pia
That’s clear simuoni wa kunishinda
Wajinga mpaka mgongo wa redioni ndo mpush ndinga
Nauza mitandaoni mitaani hunuki chinga (napendeza)
Nachafua hewa na baada ya shuzi kimba
Ama kweli Bongo ladha Bongo lala
Pengine kwa sababu hamjafika Mwitongo labda
Kwa Baba wa Taifa kukusanya blessing
Ndugu fanya upesi harakati huku kama jeshi
Sanaa yetu imezorota
BASATA boroka mashaka ni kwako sota
Kitambo tuliibiwa bila mipango
Wezi wamerudi tena round hii wana mitambo
Yule usimuache Ruby achuje
Salamu kwako muheshimiwa Nape Nnauye
Mpenda asali sa vipi muwatenge nyuki
Huu ni wangu mtazamo masela msijenge chuki

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Kwi kwi Ulamaa Professor Jay Afande

Wanakwambia 1×3 sio sawa na 3×1
Kama unabisha ukifika hospitali ukipewa panadol umeze 1×3
We meza 3×1
Unju (Bin Unuq)
B-I-G-H-D-I-D
The Don Koli Hombi
Mtu tatu ngoma moja
Mtazamo
Issam Touches
Daudi Lucas

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI