MISTARI YA WIMBO HUU

Hahahaha ah vijana sasa hivi naona wanajitahidi
Ari Mpya
Kasi Mpya
Nguvu Mpya
Ehee hata mimi nimeliona hilo toka longi taim
Au siyo Babu Ayubu
Hilo liko wazi
Jamani vijana wapewe nafasi

Si ndio sisi-M
Si ndio sisi-M
Si ndio sisi-M
Ah pisha njia
Tunaingia
Wote pisha njia
Nasema tena kwamba si ndio sisi-M
Pisha njia
Watu wazima tuongee na Watanzania

Oh yeah mtoto wa Jah-Kaya
Profesa kama Dadi japo choka zaidi ya mbaya
(On fire)
Mikasi siyo mbaya mademu nasikiliza
Kimtindo nimewafundisha tu japo sikumaliza
Inaleta maana pembeni ukiwa na mama
Na yeyote atakaye kukana masela wanaandamana
Una mengi ya kufanya kutokomeza umaskini
Kuhusu swala la vijana na UKIMWI uko na mimi
Hujajua nachokizungumzia nini
Au hujaskia albamu ya A.K.A Mimi
Na mengi ya maana ya kuongea kwa vijana
Ndiyo maana mwana nakufagilia sana
Huna mpinzani si bara si visiwani
Naamini maneno ya Komba sisi ndo namba wani

Hizi ni salam pokea zangu salamu
Ndani ya Dar es Salaam na tena ukitabasamu
Hizi ni salam toka Dom to Jakaya dot com
Sauti toka gheto mpaka home sweet home

Tuseme wakishinda upinzani labda vita itokea
Ila ni jamani amani imepotea
Ntazidi kukuombea miaka kumi uendelee
Wala usiache moyo wako wa kukumbuka wazee
Mapenzi yako kwa binti yako sawa na kwa Ngwair
Haki sasa nina imani pia utatetea japo sheria ina mkondo
Kila atakayekosea natoa pisto Dudu Baya Nice na Babu Seya
Watoto hadi wazee rika zote umekubaliwa
Wala usihofu labda siku nchi yako itapinduliwa
Nani aingie msituni na vijana wote watu wako
Mimi mwenyewe ni mmoja wa wale wenye kura yako
Shahidi ukija geto ukutani picha yako
Natamani kuona japo sarafu yenye sura yako
Kiti chako kakuachia Benjamini nakuamini son
You know what I mean

Hizi ni salam pokea zangu salamu
Ndani ya Dar es Salaam na tena ukitabasamu
Hizi ni salam toka Dom to Jakaya dot com
Sauti toka gheto mpaka home sweet home

Ninachotaka kurudisha heshima ya East Zoo
Kwa kumheshimu babu aliyepanga makao makuu
Na kila mbunge jimbo lake liwe juu
Si kusinzia bungeni tu tena miguu juu
Maisha ninayotamani huendi kuyawinda Ikulu
Basi fanya Tanzania jivunie kuwa huru
Walinde uhusiano na amani
Pia kutuokoa waige mfano wako
Kila mmoja awe staa kama aka mimi
Tuone kama taiweza naita mia tatu stini
Mimi ni zaidi ya mamiss mimi sio rahisi
DCA sijasahau na polisi
Tupunguze mbio za mchangani na mapusha
Una mengi ya kufanya kutokomeza rushwa
Kila mmoja aelewe hii situation
Ok nna mambo mengine na mimi I’m gone

Hizi ni salam pokea zangu salamu
Ndani ya Dar es Salaam na tena ukitabasamu
Hizi ni salam toka Dom to Jakaya dot com
Sauti toka gheto mpaka home sweet home

Yea mapya
Wee na East zoo
Nani mwingine wa kufanya zaidi ya hii
Zaidi ya mi
Na bado nipo na P yep
Bongo Records
East Zoo
Babu Ayubu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI