MISTARI YA WIMBO HUU

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Hadi tamati naapa muhogo sitonunua
Haikuwa Maimuna aliyekwenda ung’oa
Hadi tamati naapa muhogo sitonunua
Haikuwa Maimuna aliyekwenda ung’oa
Kapata tetekuwanga na ugonjwa wa surua
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Kula dori kula dori mshindo wa sufuria
Guriri guriri kofia inavuliwa
Kula dori kula dori mshindo wa sufuria
Guriri guriri kofia inavuliwa
Ndie mimi ndie mimi afatae ukoa
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Mtu akitaka kupa, hakuletei barua
Hukupa usingizini pasi mwenyewe kujua
Mtu akitaka kupa, hakuletei barua
Hukupa usingizini pasi mwenyewe kujua
Kwenda mbio si kupata, bure unajisumbua
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Mkato wake matege wakati anapokuja
Aliiweka dhamiri ya kumvulia koda
Mkato wake matege wakati anapokuja
Aliiweka dhamiri ya kumvulia koda
Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Kamfunge kamfunge beberu wa Athumani
Umfunge umfunge pahala panapo jani
Kamfunge kamfunge beberu wa Athumani
Umfunge umfunge pahala panapo jani
Endaeke sina hofu, atarejea ngamani
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Sina ngoa sina ngoa, kuwa daiwa sitaki
Ni mwerevu ni mwerevu, wallahi sihadahiki
Sina ngoa sina ngoa, kuwa daiwa sitaki
Ni mwerevu ni mwerevu, wallahi sihadahiki
Pambanua pambanua, viwili havipendeki
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI