MISTARI YA WIMBO HUU

Hivi nyie ma MC mnachoimba kitu gani
Mara Bangi mara matusi sa ndo muziki gani

Hii ni Hip Hop (hop)
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi kabane pua nyumbani

Hata bibi yangu mi aliniambia
Mwanamke anahitaji kubembelezwa
Kupeti peti matunzo pia
Ukienda rafu utampoteza
Muziki ni mfano wa binti muzuri
Na ndo maana namtunza kwa vazi la utuli

Ah piga kimya we ndo hufai kabisa hauna maana
Wabana pua kila siku mnalogana
Bibi yako alikuambia muziki ni kama binti
Mbona unawachezea unawatema kama Big G
Mara Wema mara Jokate mara Naj mara Penny
Je mnafanya muziki mpate mabinti

Uuhh hata wazee wa zamani walishasemaga kazi na dawa
Cha muhimu jukwaani ni kuhakikisha wanapagawa
Ule mchezo wa kuringa ringa ndo huwa wanadata
Badilika usiwe mjinga utawakamata

[Hook – Diamond & Ney Wa Mitego] Hivi nyie ma MC mnachoimba kitu gani
Mara Bangi mara matusi sa ndo muziki gani

Hii ni Hip Hop Hop
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi kabane pua nyumbani

Mziki wenu ushirikina ndo umetawala
Q-Chillah analalama anasema umemloga
Mganga wako aliyekutoa umemkimbia hujamlipa
Bila skendo za magazeti basi husikiki

Ah mi ni mti wenye matunda milele siogopi kupigwa mawe
Ubaya wenu wengi kina Kayumba elimu mlitupa sandakalawe

Bado hujanishawishi Bongo flava inanipa kichefuchefu
Kwanza nyie malimbukeni wa umarufu
Mnaleta maringo mpaka kwa mashabiki
Wabana pua nyie watoto sio ridhiki
Mnavaa nguo za dada zenu zinawabana mapaja
Nyie makakaduu

Ah nyie watoto mchelemchele (haya matusi bwana)
Kwenye show viuno mbelembele (mbona unatutukana)
ah nyie watoto mchelemchele (haya matusi bwana)
Kwenye show viuno mbelembele

Nimewanyamazisha brazameni vipi we bado unabisha

Hata mimi nina mengi ninayajua
Ila we mtemi utaanzisha utata
Michezo yenu kutoboa pua
Bora ninyamaze usinipige mbata

Hivi nyie ma MC mnachoimba kitu gani
Mara Bangi mara matusi sa ndo muziki gani

Hii ni Hip Hop (hop)
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi kabane pua nyumbani

Hivi nyie ma MC mnachoimba kitu gani
Mara Bangi mara matusi sa ndo muziki gani

Hii ni Hip Hop (hop)
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi kabane pua nyumbani

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI