MISTARI YA WIMBO HUU

2011 nakuchukia, ulifanya niporwe demu
Kisa pesa sikuwa nayo, zilizagaa kila sehemu
Konde nilipiga moyo
Ulimtesa baba yangu kutwa kushinda mahakamani
Uliuvuruga ubongo wangu, chuo sikutamani
Mwakyembe akawa hoi, na sichoki kumuombea
2011 na hapa nakuchukua, Mr Ebo kama ndoto, leo hatupo nae
Five Star matumbo joto, pengo lao nani akae
Bora upite bora uende, tuliobaki tusonge
Umetesa wamachinga, japo Mbeya nyumbani kwangu
Jangwani na mafuriko, labda mipango ya Mungu
Umeleta marafiki, japo wengi siwaelewi
Wanafiki, kuzua hawachelewi
Pesa nyingi ulizuia, hata katu sikupata
Jina tu lilinisaidia kwenye viwanja vya bata

Nikiwa street na machizi tume-chill tunabonga tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa ghetto na my baby tuna-hug na ku-dance tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nigga I hate you
Nakuchukia mwaka jana!
I hate you
Nakuchukia mwaka jana!

Wengi wao hawaamini, japo kocha waliletewa
Taifa stars wapewe nini? Kwenye challenge wakazomewa
Gaddafi king wa Libya, leo hawapo naye
Afghanstan nako msiba, Osama hawapo naye
2011 mwaka wa vioja, sio kwako labda kwangu
Na haya mawazo yangu
Nilipata simu ya vitisho nkatishiwa maisha yangu
Ah! Usinikoshe naapa kwa jina langu
Masoko ya biashara vya vilio vilitawala
Kila siku tu moto, masoko yanaungua
Wakubwa mpaka watoto mabomu yanawalipua
Nazungumzia Gongo La Mboto, nani asiyejua?
Marlaw kaweka Besta ndani, basi Iringa oya oya
Leo niko na Manecky, na ngoma iko on fire
Diamond mtoto wa Tandale, sio kwa uchawi wala ndumba
Labda yalimcheza machale, akatoa pete ya uchumba

Nikiwa street na machizi tume-chill tunabonga tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa ghetto na my baby tuna-hug na ku-dance tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nigga I hate you
Nakuchukia mwaka jana!
I hate you
Nakuchukia mwaka jana!

Niko hapa swagga zangu ziko full bro
Yes, Bizness and I run the show
They like what, what more
Baada ya kesho kutwa, ni mtondogoo
Niko hapa swagga zangu ziko full bro
Yes, Bizness and I run the show
They like what, what more
Baada ya kesho kutwa, ni mtondogoo

Nikiwa street na machizi tume-chill tunabonga tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nikiwa ghetto na my baby tuna-hug na ku-dance tu
Nakuchukia mwaka jana!
Nigga I hate you
Nakuchukia mwaka jana!
I hate you
Nakuchukia mwaka jana!

Wabongo walikosa heshima
Takwimu zinaonyesha tu
Labda kwa sasa ndo lazima
Maana wanawarudisha full ah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI