MISTARI YA WIMBO HUU

Mali ni nyingi nyumbani
Kipi kimekukimbiza
Ona babio mamio
Wote wanakulilia
Mtoto peke yako nyumbani
Kipi kimekukimbiza
Ona babio mamio
Wote wanakulilia
Ndani ya Dar Es Salaama
Ulikuja bure
Tena kimwana
Kimwana hujui kuchuna
Na zile lawama
Za wale walokuzoeza
Ulikuja jana
Na leo tofauti sana

Tena bora yule wa jana
Wa leo tofauti sana
Dakika mbili mbele nyuma
Kichwa kinauma
Tena bora yule wa jana
Wa jana leo wa jana
Dakika mbili mbele nyuma
Kichwa kinauma
Oyayee
Mbona unawatesa sana?
Omamee
Mbona unajitesa sana?

Ukaanza kulewa
Madawa
Kuvuta kwa sana
Ndani ya Dar es Salaam
Mambo matamu
Hayakukuisha hamu
We bado mtoto
Kwa mama
Hujayajua mengi
Mwenda tezi na omo marejeo ngamani
Amesema sana mama
Dunia tambara bovu
Kuna asali na shubiri
Ujana giza na nuru
We mwana wewe mwana
Mwana jeuri sana
Ulichokifuata hukupata
Umekosa ulivyoacha
Kwa baba yako mwana
Na mama yako mwana
Kwa vichache ulivyovitaka
Ni vingi ulivyoacha

Oyayee
Mbona unajitesa sana
Omamee
Mbona unawatesa sana

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU