MISTARI YA WIMBO HUU

Ayaah
Boy David
Mavoko

Mmnh
Kunani mboni zinaumia
Kuna mengi yanayonikwaza
Nalalamika ndani huku nalia
Japo usoni mi nachekaga
Nasikia mapenzi kikohozi
Ombeni nakonda na TB
Almanusura uzima nisije kata kauli
Na kumuacha siwezi kwa mutima kashakuwa nguli
Kanifinyanga mazima penzi limebaki kivuli

Japo pombe nakunywa cha ajabu silewi
Zinazidisha mawazo haki ya Mungu sielewi
Mwenzenu pombe nakunywa cha ajabu silewi
Zimezidisha mawazo mawazo

Nami naimani nawe
Naimani na
Naimani we ndo mtuliza mawazo
Mi naimani nawe
Naimani na
Naimani we ndo mtuliza mawazo
Sina kiranga penzi si nguo
Kuazimana haramu
Na ikibidi mueleze
Nilishafungwa chunga chungio
Kinachokupa utamu ndo kitakupa mawenge
Napepesa macho ili ning’amue lolote
Mapenzi ni utundu anaeza akaachwa yeyote
Kuonja sunaah mi njonjo sinaa
Ukweli unaempenda ndo anauma

Japo pombe nakunywa cha ajabu silewi
Zinazidisha mawazo haki ya Mungu sielewi
Mwenzenu pombe nakunywa cha ajabu silewi
Zimezidisha mawazo mawazo

Nami naimani nawe
Naimani na
Naimani we ndo mtuliza mawazo
Mi naimani nawe
Naimani na
Naimani we ndo mtuliza mawazo

Mwenzenu kauli mi sina (mama wee)
Yakinizidi nazima (mama wee)
Nashindwa kusema (mama wee)
Ikibidi umwambie
Kanikoleza mazima (mama wee)
Hakuna alichoninyima (mama wee)
Amenitema mapema (mama wee)
Ikibidi umwambie
Kesho nampa na bima (mama wee)
Anitulize mutima (mama wee)
Nimpe lunch na dinner (mama wee)
Ikibidi umwambie

Mama wee
Mama wee
Mama wee
Ikibidi umwambie eeh

Aah B Daddy

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI