MISTARI YA WIMBO HUU

Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia
Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia

Nimezaliwa tarehe 3 87
Sijawahi kuvaa kiatu alichonunua baba
Kakataa katukatu kunipa msaada
Tangu darasa la tatu mimi dawada
Ni shida zilizidi darasa la saba
Nikaamua niache shule mi nianze kukaba
Mama akawa anajificha kufanya ukahaba
Sababu matatizo ukata unakaba
Kila anaepita mi namvizia
Tale akipita tu mi namuibia
Alinisikitisha mimi mama Rugia
Nilimpiga akazimia nikamuibia
Nikajua nimeua kutwa nawaza
Kesho magairi ya push mie wa kwanza
Nasita kurudi kwa Mungu mi ntafukuzwa
Nisamehe jamani nishajifunza

Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia
Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia

Nasema roho ili-change nikawa kama mdudu
Sili vya kuchinjwa nashindia vibudu
Roho ime-change nikawa kama mnyama
Mi nalazimika vilivyoshindikana
Roho ime-change ikawa kama mdudu
Sili vya kuchinjwa nashindia vibudu
Roho ime-change ikawa kama mnyama
Mi nalazimika vilivyoshindikana

Tunda acha kulia
Usikonde kwa kujutia
Haya yote uliopitia ni mitego tu ya dunia
Maadam umetubu kosa Mola yupo anakusikia
Aminia
Penye nia basi pana njia pia
Mara nyingi mtenda maovu kesho anageuka mwema
Kumbuka alisamehewa muovu Maria Magdalena
Mungu wetu rehema
Bora umetubu mapema
Watu watakusengenya wengine watakusema
Basi piga moyo konde fanya kazi kwa bidii
Tena piga goti uombe ujasiri na utii
Kumbuka wewe una shida wapo wenye shida zaidi
Amini we ukishiba wapo wenye njaa zaidi
Daima kumbuka kutoa na kupokea
Sisi wote binadamu hakuna asiyekosea
Usipotee lost da way muombe Mungu akuongezee
Fanya yale yalio mema keep hustling every day

Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia
Sina raha maishani mie nalia
Kwa dhiki na mateso mie nalia (naumia)
Toka mtoto mpaka mkubwa mie nalia
Ooh eeh nalia

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI