MISTARI YA WIMBO HUU

Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nampenda penda  (naaani) msichana mmoja  (naani)
Mweupe kidogo (naaani)
Nampenda nampenda nyuma kajaza  (naani)
Kifuani — (naani)
Anakwenda kwa pozi naani
Nampenda nampenda

Nampenda dem mmoja awe Mtanzania
Awe na sifa za kweli niweze jivunia
Nijue wapi kazaliwa wapi katokea
Ndugu jamaa wazazi nipate waelezea
Uzuri wa sura yake uendane na tabia
Apendwe na watu c makumi bali mamia
Dada zangu wazazi wasije kumchukia
Waseme mbona sisi awali tulikuambia
Ntampenda dem mwenyewe awe mweusi kidogo
Hata kama mweupe isiwe kwa mkorogo
Awe mnyisanzu mnyakyu mnyalu c mgogo
Hapo ntapata raha kachaa c kidogo
Niwe kwake moyoni asiwe kwangu mfukoni
Eti umaarufu na madini yangu shingoni
Dem yamdatishe anase kwangu mtegoni
Ntapochalala dem aingie mitini
Sijui nani mkweli sijui nani nimwamini
Ila namwomba mungu roho tu ya imani
Nimpate mmoja mpenzi tu nimwamini
Nimvike pete ndoa kitu cha thamani
Utajiri umaskini ndani ya penzi ni matokeo
Kila mmoja kati yetu atambue jambo hilo
Isije siku za usoni ikaleta kimeo
Lakini nakuamini huwezi kuniacha mwenzio
Utabaki wangu nami ntakuwa wako
Kile kilicho changu mpenzi hicho ni chako
Bega kwa bega nami niko nyuma yako
Mike tee na nature haki ya mungu hatutoficha

Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nampenda penda  (naaani) msichana mmoja  (naani)
Mweupe kidogo (naaani)
Nampenda nampenda nyuma kajaza  (naani)
Kifuani — (naani)
Anakwenda kwa pozi naani
Nampenda nampenda

Hewala bwana wacha me niseme sana
Hata nikificha kwangu haitoleta maana
Ni kheli niwe mkweli muwazi anijue vizuri
Ili akipata nyeti za uzushi awajibu kiburi
Nafaham unafaham binadam sote dhaifu
Vizingiti ni vingi mpaka me nikuite wife
Imani uvumilivu pia uaminifu
Vyote kwa pamoja vyahitajika maradufu
Mikufu sarafu isiwe kipimo cha mapenzi
Kunikubali mnyalu nidrive bima au benzi
Hizo ni fikra potofu tena tu za kishenzi
Naahidi kwa kila khali mimi nitakuenzi
Nataka uwe simple wabaki na mshangao
Wale unaofanana na usiofanana nao
Nikizuka nawe msichoke wote wabaki ooh
Dem msomi ngeli no anaongea kikwao
Mfano kukataa anasema ndeema
Kila sehem nikimgusa anaheeema
Kusema toka hapa anasema hege ipa
Ngoma ikikataa anasema imenyopa
Asante ntakufundisha wewe kusema ndaga
Hivyo ndivyo mapenzi ya kinyalu yanavyokwendaga
Tuombe uzima vyote me ntatimiza
Ukiniona mike tee satisfaction guarantee

Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nakupenda
Na sifa nakupa  (Mnyakwibata)
Usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu
Nampenda penda  (naaani) msichana mmoja  (naani)
Mweupe kidogo (naaani)
Nampenda nampenda nyuma kajaza  (naani)
Kifuani — (naani)
Anakwenda kwa pozi naani
Nampenda nampenda

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI