MISTARI YA WIMBO HUU

Majani
Temba hapa

Nampenda yeye ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye
Ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye

Sikujui hunijui lakini ujue mi nakupenda
Mungu akipenda tutaishi kama wapendwa
Kimoyo naongea kwa huyo mtoto nilikolea
Siku niliokutana nae ilikuwa balaa alaa
Mtoto ana kila sifa kila kigezo wacha mchezo
Chuchu ziwa konzi kiboko kwa mapozi
Usoni no pimples macho yanaita
Akinywa soda unaiona kwenye koo ile inapita
Nikamsogelea ngojea nikaanza kumuuliza
Binti hujanijua vizuri
Sikujui bwana
Hebu tuliza mawazo na akili unaweza ukawa unanijua
Na kunitambua mi mtoto wa kishua
Mengi ni kaka angu Bakhresa ni mjomba wangu
Binti hataki kuingia line sijui nini anawaza
Na mi navyomtamani nikimpata ntamchakaza
Nikampa tena na hii
Channel 5 kwani ile nayo huijui
Naijua
Ile nayo ni yetu na Seki ni mfanyakazi wetu kwenye ile TV yetu
Anataka kuondoka nikamshika mkono
Nikamwambia tulia basi nikuagizie kinywaji makulaji
Nyama rost mbuzi kachumbali iwe shwari
Mtoto anaanza kunielewa anatabasamu kwa mbali
Kumbe ye mwenyewe mambo yake super sio kitoto
Ana mkoko wa maana huyo ananichanganya
Mi nampenda yeye yeye mwenyewe
Ananipa kiwewe yeye mwenyewe
Akanipa contact; e-mail namba ya simu
Simu yake ina full dola
Ha-beep hatumi message ye anapiga tu
Mnachonga tu tu tu tu
Siku nilioenda kwao ilikuwa mshike mshike balaa
Hata sikuingia niliishia kuchungulia
Yule nikaishia

Nampenda yeye ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye
Ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye

Huyo mtoto huyo huyo binti huyo
Mmh kwao walinzi wakali hatari hatari
Nikampigia simu huyo ananirushia stimu
Analeta mapozi kesho tukutane Nandoz
Sikufa moyo kesho ikafika
Nandoz nikafika tukawa tunaburudika
Bado mtoto hanielewi anataka kupajua kwangu
Akaone mambo yangu
Sikutaka kumficha lakini moyo unasita
Vyote nilivyomtajia kwangu atavikuta
Au ntagonga ukuta kachaa ntaumbuka
Hao tumefika home nikamkaribisha kwa makeke
Karibu karibu mgeni jisikie uko nyumbani sebuleni
Kwa kuwa umekuja leo we sema nini unataka
Chips kuku
Nkamwambia Kwa jinsi ulivyochoka poza kiu na hii soda Coca
Halafu tutatoka
Mmh akaropoka
Anadai soda haipandi anamaanisha anataka bia
Nikamletea akanywa wee mpaka zimemshinda
Mara acheuwe arembue jicho legelege aah akawa bwege
Kumbe kitu mwake mwake mwake mwake baba ake
Ilikuwa ni jioni jioni kile kigiza cha usoni
Mapenzi ni kama upofu hata mbele hatuoni
Lager zimemshinda yuko hoi kitandani
Muda ulivyofika umeme si ukakatika
Utasema Tanesco walijua kama mi leo ntaua
Umekuja kuwaka tumechoka nyakanyaka
Utasema punda kabeba mizigo au meli imegonga ukingo
Sikumpiga single haniletei tena maringo
Kachaa anavyonipa bingo lazima nikatoe single
Ah Majani
Super dupa producer man

Nampenda yeye ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye
Ye ndo yeye
Wala siwezi kwenda kwa mwingine
Ye ndo yeye
Wote wanajua mi nipo na yeye

Ye ndo yeye
Ye ndo yeye
Ye ndo yeye
Ye ndo yeye

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI