MISTARI YA WIMBO HUU

Hip Hop ni vile unavyoishi rap ni vile unafanya
Sikio la kufa zibuka upate sikie mawazo chanya
Naweza nisile nyama ila nkazuga tu na toothpick
And truth is utaenda jela ukimpa mimba school kid
Fikiri zaidi ya reason unapo-doubt
Stress zinapozidi vaa buti toka out (out)
Napiga A+ kwenye paper hii
Watu wananyooka Segerea penitentiary
Achi waamini bwana awe nanyi
Rambi rambi hazimpozi machungu mfiwa msibani
Inaweza isilete money paper ikaleta maana
Kuwaingilia wanyama sio kitendo cha kiungwana mwana
Mungu ni mwema kumba nyoka kaumba kifo
Usimchezee mwanamke wa mjeda utaliwa jicho
Na ngoma haina remedy nina energy
Na weledi ulale pema John F Kennedy
Wanasema Stereo verse foka
Nenda less tiredless bless less rocker
Bora ujinga kuliko elimu isiyotumika
Mi ni uzito usiopimika
Ngosha

Nisome mi ili ujione ukii-reflect rap science
Tone la manii lime-create huyu giant
Higher like a lion zion na pia define
Nahofia ku-retire hadi ya ubaya ta-backfire kwa client (ye ni knowledge)
Kuipata you need to learn
Na uki-practice utakuwa na skills ka hizi hauoni
Trust huletwa na doubt ka kazi na wadau
Nafasi za kuwakachu wamekaa manyang’au
Na nasikia hamtaki kick tu mnataka na snare
Mnapaka mnaongea mmedata au ni utata umewaenea
Blast for me the last word for my nigga
Niko fast homie niache nipate uboss wa eight figures
Niliyoyapitia ni makubwa future iko perfect
Niko mbele ya muda leo nai-future kwenye past tense
Kuna tofauti ya ntakula nini na nini ntakula
Ukiona nusu uchi stejini ujue wameshindwa kuuza sura

Wanaongea walichosikia mi nasema nachojua
Na najua kuwa usipojua haitonisumbua
Wanaongea walichosikia mi nasema nachojua
(Nasema nachojua)
Wanaongea walichosikia mi nasema nachojua
Na najua kuwa usipojua haitonisumbua
Wanaongea walichosikia mi nasema nachojuah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI