MISTARI YA WIMBO HUU

Me ndio Raisi wa Manzese yule tozi kasanda
Manzese mikono juu naiongoza kamanda
Wanangu nyongeni ganja msiogope polisi
Ila tu msile unga mtapoteza nafasi
Me ndio gangster rapper na kiboko ya marapper
Wanaleta ushindani mwishoni wanatoka kapa
Me natengeneza hela wao wananuka vikwapa
Eyo Mchomvu wape salam kubum kubam
Waambie watakufa nao mziki umebadilika
Napenda mnavyonidisi wala hamnitishi
Wala Diamond we si mtoto wa Kigoma
Mpe salamu Zitto Kabwe mwambie afanye siasa
Aachane na Bongo Fleva huku hatumtaki kabisa
Maneno mengi propaganda hajui kutekeleza
Kigoma All Stars tayari kawatelekeza
Naongea na RizOne eyi RizOne
We si mtoto wa Rais RizOne
Mwambie dingi yako masela hawamuelewi
Wamakonde wa Mtwara hawataki tena korosho
Wanataka gesi si mtawauwa kwa mkong’oto
Nani rafiki wa Lowassa peleka salamu
2015 nataka agombee uraisi
Nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi

We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao

Sina beef na polisi Mbunge wala raisi
Hizi ni salam tu nataka tuishi peace
Mkimaindi amna noma
Sio muelewa kula kona
Hizi salam toka bongo nataka zifike kenya
Uganda hakuna matata najua ngoma inapenya
Mambo vipi CCM mnasemaje Chadema
CUF bado ngangari au tayari mshabuma
Na salamu muhimu ziende kwa watu maalum
Nani nimtume kuzimu afikishe salamu
Kwa Kanumba na Ngwair
Siku ya misiba yao kuna watu wamepigaa hela
Wanamiliki magari wameota na vitambi
Kwa hela za rambirambi
Kwa majina nawajua mkizingua nawataja
Msisitizie na kanumba Baada ya yeye kufa
Na bongo movie imekufa haiuzi kabisa
Hizi salamu ziende kwa Madam Ritha na Bongo Star Search
Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi
Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani
Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani
Milioni hamsini zao anazila nani
Acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani
Tanzania bila uchafu kumbe inawezekana
Yoo Jakaya mualike tena Obama
Japo ujio wake kwa wengine ni lawama
Walalahoi wenzangu mishe zao zinakwama
Nani nimtume Dodoma afikishe salamu bungeni
Kuna wabunge vilaza bungeni wao wanalala tu
Na wakiamka kila hoja ndio tu
Kuna vilaza part two wao matusi na kulumbana tu
Mawaziri vivuli wana kazi gani
Wana maana gani
Wana faida gani
Wabunge Viti Maalumu wana kazi gani
Wana faida gani
Mbona mi sielewi

We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI