MISTARI YA WIMBO HUU

Kutwa viguru njiani
Majirani wote wamekuchoka
Mara chumba cha fulani
Mtu gani we kwako usiokaa
Washinda vibarazani
Vya wenzako kuropoka
Ukome mwana fulani
Ona uso ulivyo kukoboka
Sio mwisho vibaoni
Hadi kwenye vigodoro
Usio na haya usoni
Kote wazua migogoro
Hivi we haujioni
Kuwa una kasoro
Usio mchana jioni
Si wa juzi, si tomorrow
Sio mwisho vibaoni
Hadi kwenye vigodoro
Usio na haya usoni
Kote wazua migogoro
Hivi we haujioni
Kuwa una kasoro
Usio mchana jioni
Si wa juzi si aah!

Nasema nawe (nasema nawe)
Nasema nawe (nasema nawe)
Nasema nawe (nasema nawe)
Usio haya nasema nawe
Umezoea (nasema na wewe)
Kunichezea chezea (nasema nawe)
Umezidi (nasema nawe)
Zidi, zidi (nimechoka nasema nawe)

Huna haya ka kibakuli cha vumba
Popote unajitokeza babu eee haa we kichoji tu
Unaingia kwenye kundi la ninga utachanika mabawa

Ah zingifuri zingifuri, ungezinga mahala ukakaa
Usio mila desturi, usio jua tongozwa ukakataa
Usio hiyana fedhuri, uongo umekujaa
Kujifanya mashuhuri, kumbe chaka umechakaaga
Mwenzako mi ni turufu, si garasa
Mwenye nyota ya umaarufu, si kupapasa
Tena jokari la nguvu pa karata
Lile hodari maguvu si kwasa kwasa
Ooh mwenzako mi ni turufu, si garasa
Mwenye nyota ya umaarufu, si oza koza ah

Nasema nawe (nasema nawe)
Nasema nawe (nasema nawe)
Nasema nawe (nasema nawe)
Usio haya nasema nawe
Umezoea (nasema na wewe)
Kunichezea chezea (nasema nawe)
Umezidi (nasema nawe)
Zidi, zidi (nimechoka nasema nawe)
Nasema na wewe (wewe)
Nasema nawe
Nasema nawe
Nimechokaka nasema nawe

Wewee umejifunza ngumi leo wataka upigane na Tyson?
Haa!

Ale kata kata katatae katika si
Kata oh teteme teteme (kata)
Wenye kusema waseme (kata)
Ale kata, kata katatae katika si
Kata kiuno chako mwenyewe (kata)
Mola amekupa wewe (kata)
Tena vya kiri kirai (kata)
Nipe vya bara na pwani (kata)
Vile vya nje na ndani (kata)
Tumkomeshe fulani (kata)
Tena vya kiri kirai (kata)
Nipe vya bara na pwani (kata)
Vya nje na ndani (kata)
Akome fulani (kata)
Mmh!

Halooo haa!
Utavunjia ma-apple mwaka huu
Maana nazi zimepanda bei eh

Thomas!
Nasema nawe (ona wewe)
Nasema nawe (mimi nawe)
Nasema nawe usio haya nasema nawe (wewe)
Nasema na wewe
Nasema nawe (nawe)
Nasema nawe, nimechoka nasema nawe
Umezoea (nasema nawe)
Kunichezea chezea (nasema nawe)
Ooh nasema nawe
Usio haya nasema na wewe (nasema nawe)
Nasema na wewe (nasema nawe)
Nasema na wewe (nasema nawe)
Nasema nawe, nimechoka nasema nawe ooh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI