MISTARI YA WIMBO HUU

Ndoa – Aslay na Hadija Kopa

Ah haa
Ndoa ndoano babu we
Ukijishebedua itakubana

Eeh mama tarumbeta
Mwali anameremeta
Sifa ninazopata
Aslay naozesha leo
(Baba harusi hongera)
Ndoa ni jambo kubwa mwanangu
Kaitunze heshima yangu
Chozi linanitoka mwanangu
(Pole we)
Siamini macho yangu
(Ndo hivyo)
Babu harusi
Mshike taratibu
Usije ukafuta piko
Haraka ya nini wakati huyo ni mali yako
Mwanangu uchecheme
Ulofundwa usiseme kwa watu
(Usungo huo)
Maneno umungunye
Ya chumbani usiwape faida watu mwanangu

Ndoa
Usitie doa (mwanangu mwanangu)
Ukitia doa ndoa
Utanitia haya
Ndoa
Usitie doa
Ukitia doa ndoa
Utanitia haya mwanangu

Wanawake wa kisasa
Mnajifanya mna whatsapp
Hamna muda wa kushughuikia waume zenu (mtashaha)
Mkifanya mchezo wenzio watawasapombe
Ooh oooh
Usipende kugombana na mume wako
Hata kama kuna vitu vimekukwaza
Mwanamke busara
Rudi vikizidi vituko
(Hakukutoa juu ya mti babu eh)
Hapa ni nyumbani kwako hujafukuzwa
Mashoga
Wataharibu ndoa yako
Watakupindua
Watamteka mume wako
Jitahidi
Kuwaheshimu wakwe zako
Hizo ndizo nguzo
Za kuitunza ndoa yako
Wivu usiuendekeze utakutoa roho
Lakini usiwe kama zeze
Kwenye ndoa yako
We jitahidi upendeze
Uwarushe sana roho
Ila mbali usicheze na mume wako

Ndoa
Usitie doa (mwanangu mwanangu)
Ukitia doa ndoa
Utanitia haya
Ndoa
Usitie doa
Ukitia doa ndoa
Utanitia haya mwanangu

Mwanangu seketua
Seketu
Seketu
Baba seketua
Seketu
Seketu
Majirani seketua
Seketu
Seketu
Wahuni seketu
Seketu
Seketu
Nasema babu harusi
Mmemuona
Babu harusi eeh
Mmemuona
Babu harusi eeh
Mmemuona
Aah Bibi harusi eh
Mmemuona
Oho Bibi harusi
Mmemuona
Eeh baba ya mwali eeh
Mmeniona
Mhh mama ya mwari eeh
Mmemuona

Mwanaume harogwi eh
Anarogwa kwa mambo
Mambo
Mambo

Aslay nahangaika
Nisaidie wanangu
Nahangaika
Nisaidie wanangu
Babu harusi kahangaike
Usaidie wanao
Kahangaike eeieh usaidie wanao
Bibi harusi kahangaike
Usaidie wanao
Kahangaike
Usaidie wanao

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU