MISTARI YA WIMBO HUU

Changanya akili ya kuelezwa na unachokifahamu vyema
Ukweli uwe mchungu kumeza na uwe mtamu kutema
Wengi (wengi mlibebwa)
Okay nipe tena

Changanya akili ya kuelezwa na unachokifahamu vyema
Ukweli uwe mchungu kumeza na uwe mtamu kutema
Wengi mlibebwa mgongoni hamwezi ujua umbali wa safari
Naomba mnaponiskia redioni nisome kwa hii mistari
Naufamisha ufahamu kabla ya ku-rhyme juu ya beat
Namwagika damu hii kalamu haishikiki
Bado wana bang ‘Huyu Na Yule’ na ‘DotCom’ kwenye street
So ukiniona com ujue na-overcome hits
Nahitaji stripes kwenye sneakers trees kwenye boots
Ili muwe live kwenye speakers mi nasikika hata ukini-mute
I got lyric pointed that you’re half a star
Another one it’s pointed at your weakest heart
Ile sauti uisikiayo ndani ya moyo wako ndo inaitwa kweli
Na salute poa ni ile ya adui yako sio ya kijeli
Ina tofauti na ile ambayo mchizi wako akiona hujafeli
Hata mauti nayo ufichua maradhi yake ukiwa mwisho wa reli
Mwenye akili hawezilalama ikiwa ni mjinga tu ndo aliwae
Mkatili ana raha kinyama na anaamini Mungu yuko nae
Mna sell out na hamfanyi soo the concert
Simshangai Saidi Fella ku-change fani ili atoke
Hawamaanishi wanachosema au kuongea vyenye maana
Haya maandishi nayotema yakipotea ujue una laana
Huu sio mziki wa Maybach sio mziki wa mafleva
Sikwaziki ka payback sitishiki mi brave heart
I’m talking keys like way Charles kwa A bars
Mastaa wana dead kwa fans naketi juu ya throne
Fid Q hawamwoni huyu ni Yuda na Lui Vuitton
Lord is born neno

Ilishanenwa toka Afrika hamnaga siri hamnaga siri
Naeza ficha Rock City
Ilishanenwa ka kawaida hamnaga shida hamnaga shida
Ndani ya Dar au A City

Ilishanenwa toka Afrika hamnaga siri hamnaga siri
Naeza fanana na A City
Ilishanenwa ka kawaida
Hamnaga shida hamnaga shida utata ukuda

Tuache tu-spit hizi words out ah wanawira
Wasanii wengi empty huku sio kusema mbwira
Kill love chillax usinipe dili ila
Naomba uchukue ili neno na msituite tena killers
Word yeah Izzy una hasira
Hizi sio hasira hizi ubati kwetu mila
Flow desturi ku-hustle pia ni mila
Hela hela kila kitu ni hela
Dabu wa kiaina hila ndume la kuwila
Hela hela masela na mamwela
Hizi sio zama zile hapendwi mtu anapendwa hela
Wametuzidi kwa majungu lakini sio fungu
Hilo wanapeana kindugu hilo ni tatizo sugu
Win win win jiacheni kaa juu ya mbingu
Ball till we fall hakuna mechi tunashindwaga sisi

Ilishanenwa toka Afrika hamnaga siri hamnaga siri
Naeza ficha Rock City
Ilishanenwa ka kawaida hamnaga shida hamnaga shida
Ndani ya Dar au A City

Chongo hushukuru Mungu anapomuona kipofu
Ma-emcee wa uongo hawana gundu wana-hit nangoma mbovu

Lia chakula ndani ya chungu

Harusi yako itakuwa na mvua

Mdogoni ulikuwa mtundu

Utakuwa na maujanja ukikua

Kata adui unaemmudu

Ni vyema umuombee dua
Kwa yule Mungu unaemuabudu
Ili aendelee kukuumbua
Kwa kupitia yeye kuna mengi utayajua
Na huo ndo ukweli wenyewe ambao hata wewe haukuutambua
Washikaji wengi ni wanafki ka kamasi ndani ya pua
Usipowatoa wanaganda wanaziba nafasi ya kupumua
Na ukikohoa wanatanda usoni ili usijione unajua

Njaa sio tamu kama asali

Na mkono mtupu haulambwi

Weupe ungekuwa mali

Ubuyu usingepakwa rangi
Say my name say my name

I’m sure you know my name
Niite Godson kama Nas
Nas yes I am
Nawapa neno wanadata they know who we are

Wanaojua sheria msumeno ndo hutulia

Hey Mr DJ jamii ielimike
Tupe mdundo mmoja tuwape neno watu waruke
Tusiwanyime chakula chao tutawafanya wawehuke
Hizi ndo bidhaa zinafanya mziki uinuke

Siku hizi pesa haiongei pesa inaapa
Utu umeshuka bei thamani ya pesa imepanda
Kama dunia ni shule maisha yetu ni darasa
Msijifunze kuhusu huyu na yule halafu sisi mkatuacha

Ilishanenwa toka Afrika hamnaga siri hamnaga siri
Naeza ficha Rock City
Ilishanenwa ka kawaida hamnaga shida hamnaga shida
Ndani ya Dar au A City

Ilishanenwa toka Afrika hamnaga siri hamnaga siri
Naeza ficha Rock City
Ilishanenwa ka kawaida hamnaga shida hamnaga shida
Ndani ya Dar au A City

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI