MISTARI YA WIMBO HUU

Kama umenipenda kwa njaa tutaishi kwa njaa
Yatayojitokeza usije ukalalama

Sura yako muzuri ila usitishike na sauti yangu eh
Sauti nimejaliwa tu mupenzi kwenye kazi yangu
Tena pia kuhusu na umbo langu ni kazi ya Mungu
Kama umeamua kunipenda nipende kidoti wangu eh
Mpenzi waonyeshe vile unavyolichezaga buzuki
Mpenzi waonyeshe vile unavyolichezaga buzuki
Tia shela lako upendeze Bella ntatupia suti
Wale wenye tamaa na asali watakutana na nyuki
Iyoo iyoo watakutana na nyuki

Uzuri wako fahari nalingia mwenzako usiniache
Kwenye baridi kali we ndo joto nifate nikumbate
Nitapigana kila hali nipatacho kidogo tule wote
Usinimwage tafadhali utawapa maneno waropoke
Mi najua wapo wezi wa mapenzi ya watu hilo ujue
Watakuja na mapesa kukuteka mi naomba watimue

Ila tupendane tushikane tushibane mimi na we
Ning’ang’anie usiniachie tupendane tusonge mbele
Tupendane tushikane tushibane mimi na we
Ning’ang’anie usiniachie tuvutane (tusonge mbele) mimi na wewe

Ukitaka nigande kiunoni nigande kifuani
Ukitaka nigande mdomoni elea elea elea
Ukitaka nigande mgongoni nigande kifuani
Ukitaka nigande mdomoni elea elea elea

Kwenye kitanda cha kamba wee
(Elea elea elea)
Kibanda cha manyasi
(Elea elea elea)
Umejifunga na khanga wee
(Elea elea elea)
Tunaishi hatuna wasiwasi
(Elea elea elea)

Sina haja ya kunywa mapombe nipunguze mawazo
Au nitoke mifupa nikonde kisa pesa kikwazo
Unachonifurahisha hata dagaa unakula
Vibabu vikikutingisha unakunjaga na sura
Naomba nafasi nivumilie
Mambo yakiwa safi tuzitumie
Ufe nikuzike unizike mie
Nakaribia kuanguka ning’ang’anie
Na ukisikia baridi tetema tetema mwilini mwangu
Ugali na chachandu nivumilie ndo hali yangu
Mapenzi utafaidi ila uta-miss vipesa vyangu
Aa kama nimekosea nielekeze mupenzi wangu

Ameridhika na mimi japo mboga limao oh
Hasikii haambiwi pamba kaweka za mbao
Mahaba kitanzini papa kang’ata ndoano
Namuamini hihihi hana kisebusebu
Utamu wa nini Wetu ugwadu gwadu
Namuamini hihihi hana kisebusebu
Utamu wa nini Tushazoea ugwadu

Oh bado mambo bado
Karidhika na fidodido ipo siku yatakuwa gado
Mambo ooh bado mambo bado
Katulia na fidodido ipo siku yatakuwa gado

Ukitaka nigande kiunoni nigande kifuani
Ukitaka nigande mdomoni elea elea elea
Ukitaka nigande mgongoni nigande kifuani
Ukitaka nigande mdomoni elea elea elea

Kwenye kitanda cha kamba wee
(Elea elea elea)
Kibanda cha manyasi
(Elea elea elea)
Umejifunga na khanga wee
(Elea elea elea)
Tunaishi hatuna wasiwasi
(Elea elea elea)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI