MISTARI YA WIMBO HUU

Umesahau ulipotoka, hujui unapokwenda
Ukapata kiburi kuona mi nakupenda
Nilikuthamini na letu penzi kulienzi
Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi
Kumbuka nilikukuta kijijini sitimbi
Umebeba mahindi na furushi la magimbi
Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji
Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji
Kigoli mwenye umbo kama la mdori
Wala sikutaraji ungepiga nami stori
Nilifurahi kuweza kukufahamu
Na nikakuahidi subiri zangu salamu
Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi
Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi
Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba
Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba
Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa
Niliapa kujua iwapo ningekukosa
Walinikabidhi nirudi nawe mjini
Na nikakusisitiza mjini kuwa makini

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana

Alikuwa mzuri mithiri ya malaika
Alipotua mjini Zubeda ni patashika
Hakika alionekana alikuwa mgeni wa jiji
NIlipovua viatu nilivikuta ndani ya friji
Alifanya vibwenga washikaji wakanicheka
Hakutaka kitanda alilala kwenye mkeka
Alipokuwa akiona magari alikimbia
Akimuona mtu kwenye TV anamuamkia
Kila alichofanya alikuwa anakosea
Nilimvumilia kwa kuwa hajazoea
Hakai kwenye sofa alikuwa anakaa chini
Mafuta ya kupikia eti anayapaka mwilini
Namnunulia soda hataki anataka togwa
Nikimletea keki hataki anataka boga
Majirani walimpenda sababu ya uzuri wake
Nasikitika mashangingi wakawa rafiki zake
Akaanza kunywa pombe alipokwenda kusuka
Usiku anatoroka tena kwa kuruka ukuta
Nilipokuwa natoka, nae nyuma antoka
Nikimtuma kitu anadai eti amechoka
Nikienda kazini ndani analeta mabwana
Magari ya kifahari yakawa yanapishana
Hakika starehe za dunia zikamtenda
Na hatimaye hata nyumbani pia akatoweka

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana

Nilipigwa na butwaa, mtaani walinishangaa
Nilikosa raha hata nafsi ilikata tamaa
Sikujua huyu binti ni mzima au amekufa
Ilibidi niombe watu msaada wa kumtafuta
Kumbe anaonekana viwanja vya kila aina
Leo yuko na mzungu na kesho yupo na mchina
Nilipata shahuku ya kutaka japo kumuona
Ingiwa niliamini moyoni ingenichoma
Kweli tulimtafuta kwenye kumbi tofauti
Ili nihakikishe kweli hajapatwa na mauti
Nikamkuta casino la wadachi na walatino
Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyo
Pechiechipinyo na pamba za mandarino
Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo
Hakika alipendeza kwa staili alizocheza
Na kila aliyemtazama alitamani kumchombeza
Kwa pozi na dharau alijifanya amenisahau
Akaniona takataka mbele ya washikadau
Ilibidi niondoke machozi yakinilenga
Shetani kashanitega na tunda langu kamega
Akapata mimba aliyempa hakumtambua
Na wote aliowafata eti wakakana kumjua
Zubeda na mimba yake hakuwa na pakuishi
Hakujua ale nini na vipi apate ridhiki
Ghafla hifadhi yake ikawa ni stendi ya basi
Siku nyingine mvua ilimnyeshea kupita kiasi
Akarudi nyumbani eti arudiane nami
Kurudi kwao hataki, mi na familia ndani

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI