MISTARI YA WIMBO HUU

Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha

Ilikuwa ni maamuzi ya moyoni juu ya mapenzi
Natafuta njia nzuri tangu zile zetu enzi
Sababu mikosi tele imeniandama mithiri ya nyuki
Na nimeamua sitoweza saliti ndoa yetu mimi
Ni maamuzi toka ndani ya moyo niamini mpenzi
Nimechoshwa na lawama nafafia maradhi mimi
Ni kwamba mapema utahaha kutafuta mwingine mpenzi
Na sitoruhusu hiyo hali itokee ndani ya yako nafsi
Naogopa maradhi mimi, naogopa ngoma mimi
Naogopa maradhi mimi, jamani

Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha

Hapana nilikua yote haya sitoweza kuyaacha mpenzi
Geuka, tazama kitandani kadi ya kopa my sweety
Sasa niamini nichoshwa na siri ya maisha ya uhuni
Na ndio sababu sitoweza vunja moyo wako, abadani
Nahisi ni upumbavu kuwa kama vile nilivyokuwa eti
Na kama nilikuwa kiziwi basi si kiziwi tena mpenzi
Mpenzi nahofia unaweza achia ngazi mapema
Na sitoruhusu hiyo hali itokee ndani ya yangu nafsi
Hayo yote ni maamuzi niliochukua mwangu moyoni
Lengo langu ilikuwa kuyaenzi yetu mapenzi
Hayo yote ni maamuzi niliochukua mwangu moyoni
Lengo langu ilikuwa kuyaenzi yetu mapenzi

Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha

Na leo my love nakuapia
Sitorudia yoyote nilokosa
Mapenzi nilio nayo ni ya kweli
Tudumishe tuwakomeshe wenye chuki
Nafsi yangu nakupa tena
Moyo wangu pia chukua
Penzi la milele liwepo baby
Sitokuacha milele, milele
Ninakikabidhi kifo oh
Utengano wangu na wewe
Ninamuachia Mungu
Kuamua wala sio walimwengu
Oh wabaya

Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI