MISTARI YA WIMBO HUU

Nimchane
Mchane
Nimchane
Mchane
Bwege tu huyo
Mchane

Adabu yako kwanza unashika mwenyewe
Kama briefcase ya pesa nalala nayo mwenyewe
Vipi umchane Shetta huu muda wa kusaka pesa
Wote tunataka kiki zingine hazina maarifa
Unamchana Dimpoz ulimpa akashindwa
Mchawi nae baki na ile nyota ya simba
Hili bonge la beat halafu hujui kuchana
Si twashona siku hizi hatumtukani mama
Nazidi kujiajiri RIP Jeez Mabovu
Nimepiga tattoo pembeni logo ya Mchomvu
Maisha yetu kama alama za vidole
Hatufanani endelea kuwa mpole
Dunia imevaa chupi binadamu was*nge
Ishiwa pesa wakuongelee kwenye vigenge
Mrudishe kwanza Siwema kisha ndo mchane Wema
Walisema nimepotea mzee nimerudi tena

Mchane
(Shi-shi-shika adabu yako)
Mchane
(Shi-shi-shika adabu yako)
Nimchane
Mchane
Nimchane
Mchane
We ni star lengo ni kusaka dough
Sio maneno kila siku hata huoni soo

Nataka nipande ndege na mimi nivae suti
Bado unabeba zege mistari yangu sikupi
Tuzo ya Hip Hop mpeni Nikki Mbishi
Ntanunua kitanda ile siku ya harusi
Unapata wakati mgumu kila ukikosa idea
Njaa ikizidi sana huwezi hata kufikiria
Maswali hayaishi kila nikiwaza siku ya kifo
Mwanaume rijali usikubali kufa bila mtoto
Njoo Dar Es Salaam kama unataka ustaa
Shangaa hela mzee usishangae mataa
Kunywa pombe utupe siri za ndani yes
Finya tonge kabla hulamba sahani
Fanya mpeleke kati Issa akamuone baba yake
Za mwizi 40 leo imefika siku yake
Salute Bongo Movie mnaleta changamoto
Rest in peace Kanumba linaonekana pengo lako
(Japo maji mazoezi sio siri ya kuwa mweupe)
Ila nyimbo za uchochezi ni laana ya mama yake

(Shi-shi-shika adabu yako)
Mchane
(Shi-shi-shika adabu yako)
Nimchane
Mchane
Nimchane
Mchane
Bwege tu
We ni star lengo ni kusaka dough
Sio maneno kila siku hata huoni soo

Nimchane
Mchane
Nimchane
Mchane
(Shi-shi-shika adabu yako)
(Shi-shi-shika adabu yako)
Nimchane
Mchane
Nimchane
Mchane
We ni star lengo ni kusaka dough
Sio maneno kila siku hata huoni soo
Bwege tu huyo
Mchane
(Shi-shi-shika adabu yako)

Unatukana BASATA umekosa idea
Mbuzi wa Pasaka zizi la simba kaingia
Hujui kuongea utaweza vipi kuchana
Una kithembe kwenye beat unahama
Kilio haki miliki rest in peace John Woka
Moja ya wadau wa mziki siwezi msahau DJ Choka

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI