MISTARI YA WIMBO HUU

Nimekusamehe lakini sitokusahau
Visa ulivonitendea Kalala ee, eh
Visa ulivonitendea Jide ee, eh
Ulinikana eh wakati nina shida
Ukasahau yote tuliofanya nawe
Wakati unaelewa hakuna bingwa wa shida
Wakati unaelewa hakuna komando wa shida
Leo nakukumbusha shida huja na kupita

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka
Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau

Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe

Rafiki wa kweli ni yule asiyekutupa eh
Kwenye dhiki na faraja mko wote, mko wote
Kwenye dhiki na faraja ooh, ooh
Uliniacha nateseka peke yangu, peke yangu
Pasipo msaada wowote kaka oh, oh
Pasipo msaada wowote kaka oh, oh

Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka

Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe

Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama Amza Kalala
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama Komando Jide
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Iyelele mama, iyelele mama, mamee aee

Lakini Mola muweza wa yote, wa yote
Kaninusuru na matatizo yamekwisha oh mama
Lakini Mola muweza wa yote, wa yote
Kaninusuru na matatizo yamekwisha oh mama

Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau
Na yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka

Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI