MISTARI YA WIMBO HUU

Nimezama ah kwa mapenzi ii
Sijui kama nitazuka
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Wenzangu nawauliza
Nini dawa ya mapenzi
Waganga nimemaliza
Kwa makombe na irizi
Wenzangu nawauliza
Nini dawa ya mapenzi
Waganga nimemaliza
Kwa makombe na irizi

Ila imo la Muweza
Ataniafu Mwenyezi
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Nimezama kwa mapenzi
Sijui kama ntazuka
Kujikwamua siwezi
Taabani nateseka
Nimezama kwa mapenzi
Sijui kama ntazuka
Kujikwamua siwezi
Taabani nateseka

Ila imo la Mueza
Ataniafu Karima
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Nimezama nimezama
Mwenzenu katika kina
Nimebaki natizama ah
La kutenda sina tena
Nimezama nimezama
Mwenzenu katika kina
Nimebaki natizama ah
La kutenda sina tena

Ila imo la Karima
Ataniafu Labana
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Nimezama nimezama
Kwenye bahari ya Huba ah
Kila nikijitazama
Moyoni napata hofu
Nimezama nimezama
Kwenye bahari ya Huba ah
Kila nikijitazama
Moyoni napata hofu

Ila imo la Mueza
Ndio mwenye kuniafu
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Naiona yangu hali
Mimi nimedhohofika
Ah aa mimi nimedhohofika

Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka
Nimezama ah kwa mapenzi
Sijui kama nitazuka

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI