MISTARI YA WIMBO HUU

Tangu nkae jela mwaka mzima umepita
Bora leo hii Tundaman umefika
Nipe ripoti za machizi maskani
Nipe ripoti za wazazi nyumbani

Baada ya hukumu mama ako akanywa sumu
Baba akafata akaugua wenda wazimu
Si unamkumbuka dada yako wa Kidatu
Sasa ni mgonjwa tumboni ana mtoto

Kwa maana hiyo dada yangu hasomi tena?!
Hivi ni nani kamuachisha mapema?
Mama mzazi alale mahali pema
Baba mzazi augue salama

Hivi ni kipi hasa kisa na mkasa
Kilichofanya mpaka sasa uko hapa
Mi nilisikia eti Spack umebaka

Kesi sio yangu, mwenye kesi amenipa

Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)

Ukilia sana Spack utaniliza
Kweli una uchungu mpaka umepitiliza
Nimeona chozi lako limeniumiza

Mpaka leo siamini nahisi naigiza
Jela hamna mwanga yaani mda wote giza
Man chunga sana usije ukatumbukizwa
Nimeona mengi mpaka leo naumia
Wanaume feki kibao wameshaolewa

Nimekumbuka mke wako kantuma
Ameniambia usimuone yuko kimya
Kuhusu watoto usihofu ni wazima
Tangu uhukumiwe na yeye anaumwa

Iii iih iih (hujatengwa!)
Iii iih iih (Marco anakupenda)
Vipi kaburi la mama limeshajengwa?
(Nimekumbuka kaburi halijajengwa)

Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)

Gereza sio kaburi embu jikaze mtoto wa kiume
Kulia lia sio vizuri unakufuru mswalia mtume
Mwanao kaja kukuona unapaswa utulie
Ana mengi ya kitaa tulia akusimulie
Hapa ni mafunzoni, so umekuja kujifunza
Hapa sio kifungoni, why uogope kufunzwa?
Usisikie ya wajinga eti jela ni jeraha
We ndo kwanza mwaka mmoja wenzio kumi wamekaa
Kwanza muda ushaisha haturuhu tena stori
Naomba urudi bwenini ila oh I’m very sorry
Ni kweli inaniuma ila mi nipo kazini
Hey, afande Maku embu warudishe kundini hao

Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)
Iii iih iih (pole sana)
Iii iih iih (nyamaza acha kulia)

Na Bonge anakusabahi
Yaani iih… Marco anakupa hi
Yaani uuh… na Bonge anakusabahi
Yaani iih… raisi wa Manzese
Uuh… na nana anakupa hi

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU