MISTARI YA WIMBO HUU

AM Records
Classic Music
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono, mkono)

Mwili kama unavidonda ukinigusa tu naumia
Kichwani mizigo ya dhambi gunia kwa magunia
Dunia sinia pakua unachoweza
Rudisha kwenye njia walimwengu washanipoteza
Mpaka leo mwanangu yupo magereza
Mtoto wa jirani anasomeshwa uingereza
Baba ‘ake Athumani amekufa mvuvi wa pweza
Wana utajiri wa imani masikini wa kifedha
Washanichimbia kaburi wanizike nahema
Washakata miti ya kivuli mifereji ya neema
Unaeza kuta unaemwamini ndio anakuwekea sumu
Hawana alama binadamu anaekuja kukuhumu
Mwili umechoka na-force tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea
Damn

Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono, mkono

Kumekucha nipo njia panda sioni hata pa kuelekea
Na kiza ndio kinatanda niendako nani wa kunipokea
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono mkono

Unajikuta uko peke yako giza kubwa kwenye mtaa
Huoni ndugu wala jamaa uliokuwa nao jana baa
Mawazo ya karaha nafsi inakosa raha
Upepo mkali na baridi bila koti la kuvaa
Najiuliza Mungu where you are, unionyeshe njia
Kelele za uchungu na hakuna anayekusikia
Usitamani kiatu changu ukikivaa hutembei
Ikiwa siku mbaya ndio masaa hayatembei
Damn

Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono
(Nishike mkono) nishike mkono, mkono

Ah
Eyoh imagine maisha ya mtoto bila ya mzazi wa kumlea
Nambie ndoto za wangapi mitaani zimepotea
Imagine mzazi wa Lulu maumivu aliyojibebea
Sometime tunaishi nje ya malengo ulojiwekea
Kifuani kama kuna moto moyo wangu unaungua
Maumivu nayohisi usitamani kuyajua
Nashindwa kupiga hatua muoga nasua sua
Maji yakiwa shingoni ndio tunakumbukaga dua
Nashindwa kuchagua kati ya mvua na jua
Kuna kitu kimemiss nawaza kukigundua
Natamani kuwa mtoto kibaya haiwezi kuwa
Vazi la dhambi nilovaa halitakati hata nikilifua
Mwili umechoka na-force tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea

Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
(Nishike mkono) nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono (nishike mkono)
Nobody see me cry all I know (nishike mkono)
Nobody by my side Mungu nishike mkono (nishike mkono)
(Nishike mkono..nishike mkono..nishike mkono)
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono eh eeeh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI