MISTARI YA WIMBO HUU

Ikiwa umeamua kunitoroka
Ikiwa unahisi kwamba hujiskii na mi tena
Na mbona imekuwa ngumu kunidokeza
Naona ni bora nilie leo, badala ya kesho
Kupenda, usipende ni kama kujitia kitanzi
Nitachimba na sururu, kwa ardhi nikitafuta penzi lako
Ni heri nipigwe fimbo kwa mwili
Sababu ntajikuna ama ntajikanda na maji moto
Maumivu ya penzi, mtu hajikuni
Wala hajikandi na maji, na hakuna upasuaji

Kama kuna kosa nimewahi fanya (nieleze)
Kama kuna jinsi tunaweza leta (mpatanishi)
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda (nielezee)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) nasema
Nitatenda (tenda) nieleze
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)

Kweli hukumbuki uliyoyafanya
Ni kweli unakumbuka tulipotoka
Sisemi habari zozote za kusikia
Bali kwa ushahidi niliouona
Msamaha mara ngapi umeshaomba na bado
Je ni makosa mangapi niliyoyafumbia macho
Mpaka leo nahisi kufika kikomo
Maumivu yanazidi ndani ya moyo
Sitaki kwenda mbali kwani uko moyoni
Nikusamehe mimi mara ngapi wee
Nieleze, mpenzi, mara ngapi

Unataka nikusamehe mara ngapi (Usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi (Hii ni ya mwisho)
Je wewe nikulilie mara ngapi (Vumilia)
Sitoweza (utaweza wee), nimechoka (usichoke)
Nimeshindwa (usishindwe), naondoka (usiondoke)
Sitoweza (utaweza yes you can), nimechoka (mmh mh)
Nimeshindwa (usishindwe), naondoka (usishindwe)

Ukihesabu mara ngapi umenisamehe
Ni kama kuhesabu ni mara ngapi mtoto kaharibu nepi
Usichoke, usiondoke, usilie
Niko hapa nakukulinda

Kama kuna kosa nimewahi fanya (nieleze)
Kama kuna jinsi tunaweza leta (mpatanishi)
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda (nielezee)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) nasema
Nitatenda (tenda) nieleze
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)

Unataka nikusamehe mara ngapi (Usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi (Ningependa univumilie)
Je wewe nikulilie mara ngapi (Univumilie)
Sitoweza (weza wee), nimechoka (yes you can, yes you can)
Nimeshindwa (usishindwe), naondoka (ushindwe)
Sitoweza (yes you can, yes you can), nimechoka (ntajitia kitanzi mamaa)
Nimeshindwa, naondoka leo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI