MISTARI YA WIMBO HUU

Sura yake mtaratibu
Mwenye macho ya aibu
Kumsahau najaribu
Ila namkumbuka sana
Umbo lake makhbibu
Kwenye maradhi aliyenitibu
Siri yangu kaharibu
Bado namkumbuka sana

Alionifanya silali, jua kali nimtafute tukale
Lakini hata kujali, darling, akatekwa na wale
Alionifanya silali, jua kali nimtafute tukale
Ila wala hakujali, darling, aka

Ntampata wapi kama yule
Nilompendaga sana
Ntampata wapi kama yule
Na anipende sana

Ai nyota, nyota ndo tatizo langu
Ai nyota, mpaka nalia peke yangu
Ai nyota, nyota ndo shida yangu
Ii nyota, wamenizidi wenzangu
Alidanganywa na wale
Wenye pesa nyumba gari
Mi kapuku hakunijali, akanikimbia
Alidanganywa na wale
Wa mapesa nyumba gari
Mie unga unga hakunijali, akanikimbia

Alionifanya silali, jua kali nitafute tukale
Lakini hata kujali, darling, akatekwa na wale
Alionifanya silali, jua kali nitafute tukale
Ila wala hakujali, darling, aka

Ntampata wapi kama yule
Niliyempendaga sana
Ntampata wapi kama yule
Na anipende sana

Bado ananijia ndotoni
Ila nikiamuka simwoni
Bado ananijia nikilala
Haki ya Mungu sio masihara

Bado ananijia ndotoni
Ila nikiamuka simwoni
Bado ananijia nikilala
Haki ya Mungu sio masihara

Hii ni sauti ya raisi
Ilomshindaga ibilisi
Kwa mwanadamu sio rahisi
Hahah kamwambie
Lazima ujue kutofautisha
Kati ya msalaba na jumlisha
Kuna X na kuzidisha
Ni cheche!

Bado ananijia nikilala
Haki ya mungu sio masihara

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI