MISTARI YA WIMBO HUU

Vipi mizigo umeshaweka tayari
Sijechelewa nkaachwa na gari
Basi jikaze usilie mpenzi
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina
Nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka tu maa

Kama watoto wakinililia (kamaa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mamaa)
Wadanganye na vibagia (wadanganyee)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (aaah aa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mama)
Na we usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirudi salama)

Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi
Ukumbuke na moyo utajawa na simanzi
Ntakapokuwa nakwenda shambani
Hafu’ niko peke yangu honey
Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah
Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani
Sina wakunitua nyumbani ntaliaa

Maneno yako yanafanya nakosa raha na mawazo
Hata mwenzako sijawahi kufika Dar huu ndo mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh
We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

Kama watoto wakinililia (kamaa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mamaa)
Wadanganye na vibagia (wadanganyee)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (aaah aa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mama)
Na we usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirudi salama)

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
Usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki

Ile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ooh

Ile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Ntarejea mama
Niombee nirude salama
Ohhh watoto wadanganye iiih uuhh
Tozane, twijalie

Kama watoto wakinililia (kamaa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mamaa)
Wadanganye na vibagia (wadanganyee)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (aaah aa)
Waambie kesho nitarejea (ntarejea mama)
Na we usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirudi salama)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI