MISTARI YA WIMBO HUU

Ayaa!
D Classic
Mmh!

Zile kelele za mto, hazitotikisa mwamba
Kama jaribio langu, kutishia mlima sawa na mate kuzima moto
Basi ungenieleza ule muda wangu ningesoma hata gazeti
Naona najidhariri kutangazia umma napendwa kumbe natendwa

Unawaambia mashosti, imeku-cost kuspend muda na mimi
Umeniwekea nuksi, ona sipati mwenye upendo wa dhati ehh

Sawa nimeumia, ila nitazoea
Jua dunia duara nawe yatakutokea
Nakuombea Mola ohoo
Akuepushe madhara
Maisha sio masihara, ipo siku utanambia ah

Basi Mwasi
Sikio la kufa halisikiagi dawa
Ya nini nikupeti peti
Kisicho riziki sili nakitupa mbali
Basi Mwasi
Sikio la kufa halisikiagi dawa
Ya nini nikupeti peti
Kisicho riziki sili nakitupa mbali

Sikukushtua haya, niliposema ‘basi nenda’ (basi neenda)
Nilijiuguza haya, niliposema mi ‘dhahabu’
Niliposema baby ‘simama’ ulizidi songaa (why?)
Nimeamini we sio binadamu ni kinyonga
Nimedanganywa utulivu wa nje
Kwa ndani unatokota
Na umeniponda kwa nyundo ulozungushwa miba nguvu tena sina eiih

Sawa nimeumia, ila nitazoea
Jua dunia duara nawe yatakutokea
Nakuombea Mola ohoo
Akuepushe madhara
Maisha sio masihara
Ipo siku utanambia ah

Basi Mwasi
Sikio la kufa halisikiagi dawa
Ya nini nikupeti peti
Kisicho riziki sili nakitupa mbali
Basi Mwasi
Sikio la kufa halisikiagi dawa
Ya nini nikupeti peti
Kisicho riziki sili nakitupa mbali

Eh eh eh yere uh eh
Eh eh eh yere uh eh

Asante

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI