MISTARI YA WIMBO HUU

Eh
Ohoo yangu
Kama itakusaidia (yangu)
Kama itakupa ushindi
Moyo wako unajua
Kama itakusaidia
Kama itakupa ushindi (yangu)
Moyo wako unajua
Usiku rafiki wa giza

Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue

Ama kweli..
Kama hujui unakokwenda huwezi kupotea
Na watu wakikimbia wanakozika
Hudondokea kwenye maiti nyama
Siku zote naamini huwezi kulala kwenye mto
Hata kama umekauka
Na ukitaka kujua mwendo wa mjinga
Mpe kilemba uone
Hili ni ombi langu, toka kwangu kuja kwako
Kama ya kwangu itakusaidia chochote
Kwenye ushindi wako, niko tayari kukupa
Ila uifuate nyumbani, wala sio mbali
Nakukumbusha ukitaka nzi wasikufuate
Acha kula vilivyooza
Chuki humchoma aliyehifadhi kwenye moyo tu siku zote
Nakuuliza unataka kuja mchana ama jioni
Maana kila njia na muda wake
Najua mara nyingi utapenda kuja mchana
Ili uonekane
Naomba nikuelekeze hivi..
Pita uwanja wa taka hadi mfereji mchafu
Kisha kibanda cha mbavu za mbwa katiza
Usisikie la mtu njiani, endelea kuja tu
Ni kioo tu peke yake ndo uonesha doa la kweli la mtu kwenye paji la uso
Katisha choo cha gunia pembeni maskani kempu
Taribani kempu
Ukisikia harufu bana pua haraka
Hapo choo kinapakuliwa
Nakutia moyo tu, njoo karibia
Unakaribia kufika

Eh
Ohoo yangu
Kama itakusaidia (yangu)
Kama itakupa ushindi
Moyo wako unajua
Kama itakusaidia (itakusaidia)
Kama itakupa ushindi (yangu)
Moyo wako unajua
Usiku rafiki wa giza

Uliza baba Ubaya aliyetoroka jela
Au mama Mwantumu anayesutwa kila kukicha
Ukiogopa kupotea uliza babu Mshuba
Kikongwe muuza bangi
Atakupa uchochoro utapita ubavu ubavu
Kila hatua utakayopiga kumbuka
Maji ya dafu hayanywewi kwenye glasi
Na siku hizi kinachopandwa kwenye changarawe
Kinakua haraka kuliko kwenye udongo
Nakuomba ukisikia KUDUM-TU TU TU TU
Kuna mtu anachezwa, endelea kuja
Ukisikia cherekooo, watu wanasasambua
Endelea tu unakaribia
Alama kubwa utakazokutana nazo
Visheti na chipsi dume, kashata na maandazi
Chapati na urojo wa ubuyu, pweza na vijiti vyake
Ukiona sufuria la supu, unakaribia
Maana nchi yenu, nchi yetu
Hapa watu pale kinyesi na kondom ndo kwetu
Hapa dampo dogo pembeni maji ya mtungi
Nyumbani huko
Chumba cha baba hapa choo cha pipa, unakaribia
Usiponikuta jua kwamba niko Ferry
Unga unga mwana kwenye samaki
Anayechafua anasafisha pa kuzitupa hana
Hapo sasa umefika, vipi
Bado unaitaka na ya kwangu ikuongezee ushindi
Kama ndio, kuna masharti mawili tu
Pitia kwa yule mama ukamuombe samahani
Na uumpe pole, kwasababu kwa kauli zako
Alipoteza kichanga chake
Na kwenye hela mkiweka picha zenu
Wekeni na za kwetu
Wakati mnatumia, mtutumie na sisi
Mwisho lakini sio kwa umuhimu
Kwenye kiapo chako cha kweli
Ongeza na majina yetu

Eh
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue

Ohoo yangu
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue

Ohoo yangu
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue

Ohoo yangu
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue
Basi njoo uichukue uichukue

Eh
Ohoo yangu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU