MISTARI YA WIMBO HUU

Yeeeah
Waacheni watoto wadogo waje kwangu
Maana ufalme wa mbinguni ni wao
J Ryder where you at
Am the pastor of this church
Am the pastor of this church
It’s Tongwe Records

Fanya ishara ya msalaba upokee haya mahubiri
Mimi ni mteule ninawaletea injili
Nina ushuhuda wa kiroho bwana yuaja msubiri
Natangaza upako na habari za mnara wa babeli
Wachungaji wanalumbana wakigombania waumini
Wanalala…wakiamka wanaanzisha dini
Hawaogopi damu ya msalaba bible wanaifanya biashara
Wewe sio  yesu hata kama baba yako ni fundi seremala
Wewe ni nani usiyekosea kila unaye muombea anapona
Hatutaki shuhuda za uwongo aminini nyote mtachomwa
Ndani ya vazi la suti unakebehi wakatoloki
Mtaleta dini zote ila RC itabaki
Hata kristo alipoponya hakutaka malipo
Akaunti yako imejaa sadaka zetu wakristo
Toba yako haijaswii halafu unajiita una upako
Siyo kila atakaye niita bwana basi ataiona pepo

We ni nani unayejiita nabii kwenye jamii
Hizi nyakati za mwisho soon atashuka masihi
Piga magoti tusali
Ameeen
Piga magoti tusali
Ameeen
Waumini wamekimbia kanisa madhehebu yanaongezeka
Hizi nyakati za mwisho cheki manabii wa uwongo
Mwana wa Adamu yuaja
Ameen
Mwana wa Adamu yuaja
Ameen

Laiti ningeweza  ningekugeuza jiwe la chumvi
Vipi unipangie  sadaka pastor gani we mlanguzi
Hakika  ilinenwa usitumikie  mabwana wawili
Siasa na kanisa kama hadithi za kaini na abeli
Kama wasabato wasiokula kitimoto wala kambale
Wanasadaki mbele ya haki wanaamini agano la kale
Mnatangaza ufahari wenu kwenye vikapu vya sadaka
Hakuna sadaka ya  kweli kama ya kumchinja isaka
Kanisa lako halifanani na ufalme wa yehova
Madhehebu yanajitenga kama  makundi ya bongo fleva
Heshima ya mkatoliki inashuka kama theluji
Dini mnaifanya miradi kwa kivuli cha uchungaji
Kanisani mnaonyeshana ufahari wa kuvaa bazee
Hekalu mnalichafua  kwa  sadaka ya pedeshee
Biblia hujaimaliza unataka uzima wa milele
Usije ukatuchoma moto kama wafuasi wa kibwetere

Hizi  nyakati za mwisho soon atashuka masihi
Wewe una mamlaka gani mpaka unajiita nabii
Kukataza waumini wasivae mapambo kwako jadi
Ili pesa wakupe sadaka na kisha unafanya mtaji
We mchungaji umekusanya waumini kwenye vijiji
Ukawaongoza sala ya toba kama yohana mbatizaji
Unabeba gunia la dhambi na yesu kumvika taji
Usiniwekee mkono kichwani huna karama ya uponyaji
Imani yako ndogo kama punje ya haradani
Uza mali zako zote pesa uwape masikini
Unatupa kiini macho unatumia gari ya kanisa
Haleluya haleluya kumbe unatuibia sadaka
Yesu hakuwa mganga wa kienyeji Japo alimponya kipofu
kwa tope la mate yake ila kwako napata hofu
ee mungu napiga goti hiki kikombe kiniepuke
Mwana wa Adamu yuaja basi tungoje ashuke

Angalieni mtu asiwadanganye
Maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema “Mimi ni Kristo”
Nao watadanganya wengi
Haleluya
Ameeen
Manabii wengi wa uwongo watatokea
Kutakuwa na dhiki kubwa siku hiyo
Je hamsadiki yakuwa hizi ni ishara kwamba  Mwana wa Adamu yuaja
Ameeen
Basi kesheni mkisali maana hamjui saa wala siku
Am the pastor of his church
Its Tongwe Records

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU

ROMA - PASTOR PERFORMANCE.wmv