MISTARI YA WIMBO HUU

Nilipokuona kaka moyo ulitikisika
Nilipowaelezea katu sikusadikika
Mbele ya Mungu kaka, daima nitakukumbuka
Kwa pendo lako la dhati, pendo lenye uhakika

Nitakuwa nawe mpenzi
Siku zote maishani
Kwani hili lako penzi
Sijaona asilani
Usikonde, usihofu
Kwengine simtumaini
Na kamwe sitakubali
We uende mbali nami

Si masihara, si utani
Kama walivyodhani
Na sasa watahamaki
Niko nawe maishani
Naapa ulimwenguni
Sitakuacha asilani
Hawatapata majibu
Ninakupenda kwanini

Nitakuwa nawe mpenzi
Siku zote na milele
Kwani hili lako penzi
Nitalienzi milele
Sitaki mwingine mwenzi
Wala mpiga misele
Na kamwe sitokubali
We uende mbali nami

Sioni wa kulivunja, na katu sitomuona
Watabaki kujigonga, lako hawataliona
Mashariki, magharibi penzi lako limwanana
Nikiugua mpenzi, kwa penzi lako ninapona

Hata wakisema sana (waache waseme)
Sitoacha kukuwaza (uh sitowacha)
Kwa kuwa tunapendana (mimi na wewe)
Muda hatutapoteza (ooh)
Yote ni yangu maisha (yangu maisha)
Hakuna wa kujihusisha (nani wa kujihusisha)
Sitokuacha asilani
Kwako mimi nimekwisha (mmh tarara aah)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI