MISTARI YA WIMBO HUU

Twende zetu tukafanye kazi
Eeehee (Ayaah)
Hehahah (limsitu la vina)
Rock city Mwanza Mwanza
Yeah, Msodoki The Son

Tena usiniletee usela kwenye kazi
Urafiki bila hela labda jela na mtaani ni usela mavi
Hii ni kwa washua na waswazi
Nalipua kishindo cha gogo huwaga hakina ukimya kwenye maji
Jua nang’aa kote, mziki unafika pote
Marafiki wasaliti ntawadiss siku zote
Sihitaji peace popote, wasanii nyota ya pipi ndo waga wananyonywa siku zote
Ah shika popote utafika tu
Underground sota maana ukitoka utafika juu
Umakini ndo kauli kuu
Sijui kuwa napoenda hotelini napelekwa na njaa ama miguu
Napenda nachopata, napokosa nachopenda
Na-enjoy kuwa hapa maana nimetoka muda haujakwenda
Penda chako ukikijenga
Kama hupati picha kesho yako basi kamera ya fikra zako ina chenga
Tukichana tusifiwe, kashfa tutupiwe
Mafanikio yenyewe hayataki tufanikiwe
Wasoweza wanabebwa nahisi kudata
Muziki hauna hela nilizotarajia kuzipata

Na raha napoikumbuka Rock City
Ilio bora kushinda njaa kuliko kushinda studio
Furaha kuchezwa mwili na mpenzi kuliko kuchezewa akili na washenzi

Popote popote kambi
Kinacho-matter ni kudaka chambi chambi
Maana siku nazo hazigandi (iihii iih)
Popote popote kambi
Kinacho-matter ni..
Maana siku nazo hazigandi

Ujuzi kama huu wapi waupate
Mapinduzi ya mabadiliko mengi hayawezi kufanywa na wachache
Nifate mapema kwa umakini
Usichukie nachosema kama hujui namaanisha nini
Ukweli unawapa tabu, haya maajabu
Je Hip Hop huwa ngumu kuliko somo la hesabu
Najionea maajabu ingawa napata tabu
Wadada wanaojiuza eti nao wanavaa hijabu
Sijiviki dharau, nimefanikiwa angalau
Tabasamu usoni napojikumbusha nilosahau
Hawariziki nyang’au, binadamu jau
Ndo maana nikikosana na marafiki napika kuku pilau
Wengi walikuwepo wamepoteza muelekeo
Wote wamekwenda na upepo
Wameridhika matokeo, wanaopambana mpaka kesho vimeo
Ndo wanasikika hawajui kuchana
Wa jana wabovu waliojengwa leo
Ukisikia unafiki ndio huo, basi acha niandike
Napoandika hazisomeki mpaka chuo
Najiongeza mizinguo, kweli elimu ufunguo
Mlango hauonekani kwenye jumba la ujinga kituo (otizogema)
Misimamo inaniongoza mzee wa kupinga hoja
Haya mapambano kwenye jiji la mzaramo ni vioja
Kwa michano watangoja (mi namba moja)
Kipato chao cha mia tano hawanitatui mi ni tatizo la laki moja

Popote popote kambi
Kinacho-matter ni kudaka chambi chambi
Maana siku nazo hazigandi (iihii iih)
Popote popote kambi
Kinacho-matter ni..
Maana siku nazo hazigandi
Popote popote kambi
Kinacho-matter ni..
Maana siku nazo hazigandi

Young Killer twende zetu tukafanye kazi
Kinacho-matter ni..
Furaha kuchezwa mwili na mpenzi kuliko kuchezewa akili na washenzi
hahahah
Ujue mi sinaga swaga kabisa
Sa sijui nimuite nani aje anipitie outro
Lakini ngoma ndo ishaisha shout out to mwanangu (KIROBOTO)
Au sio

Hii scene yaa
Ya Miss Hip Hop
Fantente vankutazanie
Young Killer saskropo saikali msitu wa vina
Yeah, hii si mmeka
Tanzaniano
Foma mwintu nontena daji baba
Hahahah Msodoooki
Power House Of Music

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI