MISTARI YA WIMBO HUU

Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai

Siri zote ametoa yeye
Ya uongo amesema yeye
Kupakaza mi sina kitu
Huyu rafiki wa mashaka
Oh oh najuta (najuta)
Amenisaliti, kwanini? Kwanini?
Nilidhani rafiki oh

Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai

Nikisema sina rafiki, walimwengu niaafikini
Marafiki sio rafiki, wamejawa unafiki
Unampa unalojua ukidhani atalitunza
Dakika chache tu kupita, kona zote kashafikisha
Rafiki upatwapo shida, atakuwepo kushika bega
Na akitoka kukupooza, ukigeuka anakucheka
Kesho kutwa ukipata pesa, wa kwanza kuyapeleka
Kwa kusema eti umekopa, huna uwezo wa kifedha
Rafiki

Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai

Oh nashangaa, bado nashangaa
Huyu rafiki, rafiki gani!
Huyu rafiki, rafiki gani?
Mwenye roho kama gazeti!
Tena gazeti la Ijumaa, lisojua mema ya mtu
Hunisema kwa mabaya tu
Kwani mimi kweli sina jema?
Rafiki huyu hana utu, anachojali ye ni pesa

Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai

Muongo rafiki huyo, rafiki huyo
Wa mashaka rafiki huyo, rafiki huyo
Mchonganishi rafiki huyo, rafiki huyo
Ameniponza rafiki huyo, rafiki huyo
Mnafiki rafiki huyo, rafiki huyo
Kaa mbali nae rafiki huyo, rafiki huyo
Leo kwangu rafiki huyo, rafiki huyo
Kesho kwa Monica rafiki huyo, rafiki huyo
Ye ni mdaku rafiki huyo, rafiki huyo
Mara kwa Sinta rafiki huyo, rafiki huyo
Nasema ni muongo rafiki huyo, rafiki huyo
Mara vingine kwa Chifupa rafiki huyo, rafiki huyo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI