MISTARI YA WIMBO HUU

Nilikutana nae pande za Kinondoni
Mida ya saba mchana ilisema saa ya mkononi
Stendi ya daladala maarufu kama Morocco
Mi natokea Mbagala naenda pande za King’oko
Ghafla nikashtuka alivyonigusa bega
Kwa gadhabu milipogeuka ni yeye nikaona shega
(Ila) Sikuamini nilipomuona kwamba ni bibi
Au msichana mdomo kushona ikanibidi
Namkumbuka nilisoma nae shule ya msingi
Ndugu hawana mpango nae tangu alipokufa dingi
Darasa la saba nauhakika hakumaliza
Usawa ulikaba akikumbuka inamuumiza
Yamemsibu rafiki ukimuona huwezi kumjua
Kachakaa hatamaniki hana viatu anapekua
Dhambi kumpa kisogo hana tiba anapougua
Shida zake tangu mdogo sasa mtu mzima amekua
Siku ikipita hajala inshaallah Mola anajua
Wapi usiku atalala ni msala anaomba dua
Anatamani kufa msalaba apate kuutua
Kafeli kujiua Mungu hajapenda kumchukua

I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high

Kumbe alipata kazi ya usafi ndani ya kanisa
Na nyumba ya mwiinjilisti aliamini nyoka wa Kibisa
Maisha yakaendelea mara zikaanza visa
Alipoguswa akalegea pasta nyavu akatikisa
Lisa aka-surrender kama mtuhumiwa kortini
Akasahau kalenda kwa utamu wa penzi ofisini
Kila starehe alitenda zaidi ya pasta na muumini
Mwazimu aligeuka mwenda aliyempenda kiongozi wa dini
Alimchengua akili na kumuondolea usichana
Mengine akaona sio dili ngono ndo tamu sana
Kakesha akisubiri maana anajulikana
Miezi ni kumi na mbili ila hata mmoja hakuonekana
Akamfungia safari pasta aliyempenda jana
Bahati mbaya hakuwa tayari kuikubali akamkana
Mbele ya umati akamuumbua sio yake wakaachana
Akamuapia angemuua endapo kwake angeonekana
Akaipoteza imani akazamia mitaani
Kwa ushetani wa pasta feki ambae hivi sasa yupo ibadani
Maisha yake hayaendi poa
Aliyemtamani amemtapeli
Mimba alifaulu kuitoa
Ila Ukimwi amefeli

I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high

Kizuri daima hakidumu
Shida kitaletewa
Suluhu sio kunywa sumu
Wherever anaenielewa
Ye nini maisha magumu kila kitu amepewa
Ukimwi hatoulaumu kwa biashara ya mwili Sewa
Masikini na vibopa ye anawapa mdudu wa karne
Kama hauna leo unakopa ye kwake mteja ni mfalme
Panda usiku panda mchana ukihitaji mwezini sana
Jeneza hofu urefu nishaukadiria upana
Wa msichana
Vidume vinapangwa toka Ukonga hadi ubungo
Msichana anatwangwa na kupetwa kama ungo
Msiogope kuzichanga anauza bei nafuu
Kashayavuka tai ya Langa matawi ya juu
Kashaipoteza dira life gumu aliopitia linamtia hasira
Future amemaliza malengo hayajajatimilika
Kifo amebakiza najiuliza kesho itafika ni patashika

I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high
I’m sitting in my room
Thinking back on you memories high

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI