MISTARI YA WIMBO HUU

Unajua nakupenda (relax)
Najua unanipenda (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Tutakuja oana (relax)
Unajua nakupenda (relax)
Najua unanipenda maa (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Tutakuja oana (relax)

Unalalamika sana umesahau hali yangu
Maisha yangu magumu
Yananipasa nijipange upya maa
Wacha nitafute chapaa
Ndoa tutafunga tu
Unavyolalamika mimi unanitia mikosi kwenye kazi
Kuna siku itafika nitakuja mama
Tulia tulia mama usilalamike sana

Unajua nakupenda (relax)
Najua unanipenda (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Tutakuja oana (relax)
Unajua nakupenda (relax)
Najua unanipenda pia (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Tutakuja oana (relax)

Mvumilivu hula mbivu
Yatupasa tuombe Mungu
Yeye pekee ndio anajua siku saa na dakika
Wewe ndio chaguo langu
Hakuna mwingine
Usilalamike sana maa mama mama mamaa
Kuna siku itafika nitakuja mama
Tulia tulia katika uchumba wetu mama

Yeh mama (relax)
Najua unanipenda sana (relax)
Niko njiani rudi (relax)
Tutakuja oana (relax)

Unajua nakupenda (relax)
Najua unanipenda (relax)
Kidumu ukipiga mwambie (relax)
Kwamba mimi namupenda sana (relax)

Nimeleta barua
Kutoka kwa Peter Msechu
Ujumbe mwengine umetoka kwa kinywa chake
Kwamba anaku-miss sana
Kwamba hakuli halali
Hana shida nyingine
Ila tu kukupenda wewe
Hana shida nyingine
Ila tu kukuwaza wewe
Najua unampenda
Pia ye anakupenda
Fujo ya nini
Mimi sielewi kabisa
Najua unampenda Msechu anakupenda
Kelele za nini Wacheni kunisumbua mimi mzee

Mama mamaa
Najua unanipenda sana
Niko njiani rudi
Haina haja ya kulalamika
Watasema vingi usisikiize
Mimi natafuta chapaa
Mimi natafuta chapaa

(Relax)
Najua unanipenda (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Tutakuja oana (relax)
Unajua nakupenda mamaa (relax)
Najua unanipenda (relax)
Nipo karibu kuja (relax)
Ntakuja kukuona (relax)

Najua unanipenda sana
Unajua nakupenda sana
Nipo karibu kuja mama
Ntakuja kukuoa
Usilalamike tena
Punguza mukari mama
Niko njiani ninakuja
Ninakuja
Baby ninakuja usilie tena
Ninakuja na pesa kibao
Nitakuoa mama
Mbele ya mashahidi wengi
Utacheka mwenyewe
Nitakapokupa pete
Pete ya ndoa yangu mama

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU