MISTARI YA WIMBO HUU
Mwanzo nilijua upo msalani
Kama sio uko utakuwa nyumba ya jirani
Nikapiga simu yako haipatikani
Ndo unapokea saa hizi mami upo sehemu gani
Kwanza kabla sijajibu naomba samahani
Ile njaa ya tumboni imepanda mpaka kichwani
Sijakuaga ila jua ndo nipo njiani
(Ningependa niwe na wewe ila upo utumwani)
Sijakuaga ila jua ndo nipo njiani
(Ningependa niwe na wewe ila upo utumwani)
Ina maana umechoka sasa wala ni mapema
Izo shida zimenichosha ntazeeka mapema
Ooh
Ni kweli ndani kuna masufuria
Chakula hakuna nini nitakupikia
Na kama tukipika basi bamia
Kutwa nzima na njaa kama ngamia
Nguzo ya upendo kusubiria
Kwa nini umeshindwa ni vumilia
Na mimi mbona nina kupigania
Mami rudi nyumbani mola atajalia
Aah siwezi (kwa nini)
Sirudi (sababu gani)
Siwezi (aah)
Sirudi
Nguo zangu zilivyochoka kama tambara ya deki
Zimetoboka unaweza kusema neti
Huishi madeni dukani kwa Mangi mpaka benki
Na ukirudi nyumbani mfukoni huna senti
Anapanga mola kupata kukosa ivi
Akinipa nashukuru na kama nikikosa sibishi
Kwenye swala la mapenzi mali sio kitu iyo
Ukweli wa mapenzi moyo kila kitu iyo
Ina maana umechoka sasa wala ni mapema
Izo shida zimenichosha ntazeeka mapema
Ooh
Ni kweli ndani kuna masufuria
Chakula hakuna nini nitakupikia
Na kama tukipika basi bamia
Kutwa nzima na njaa kama ngamia
Nguzo ya upendo kusubiria
Kwa nini umeshindwa ni vumilia
Na mimi mbona nina kupigania
Mami rudi nyumbani mola atajalia
Aah siwezi (kwa nini)
Sirudi (sababu gani)
Siwezi (aah)
Sirudi
No comments yet