MISTARI YA WIMBO HUU

Nndoto, nndoto, nndoto, nndoto
Nndoto, nndoto, nndoto, nndoto

Mimi ni mvuvi toka kaskazini baharini
Sina chochote mfukoni
Sihusihani kabisa na madini
Hivi ntakupata na nini?
Usiku kucha nakesha mtoni
Haiba imepotea usoni
Mapenzi hayana makazi, malazi
Utayapata popote duniani

Ila na imani toka moyoni
Umeiteka ramani
Tena uletwe mzani upimwe upendo wangu
Mi ntatoka number one
Ila naimani toka moyoni
Umeiteka ramani
Tena uletwe mzani upimwe upendo wangu
Mi ntatoka number one
Haya

Mi ka samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)

Ni mwenye mapenzi yako, mjuzi wa thamani yako
Nikupe samaki hautaki
Nuru lahai wa ubani, mtoto wa allua tani
Hata kwenye baraza ntashtaki
Si kwa wali mkavu na kwa chukuchuku chee
Nakuletea jodari ufurahi
(Mzuri wewe)
Usio na fikra chakavu nkiondoka ntakupa neno byebye
Wangapi wenye wingi wa mali
Mapenzi yao ni mafuta na maji?
Tamati nitakupa samaki
Kuhusu upendo mi ni kama dibaji
Wangapi wenye wingi wa mali
Mapenzi yao ni mafuta na maji?
Tamati nitakupa samaki
Kuhusu upendo mi ni kama dibaji

Ila naimani toka moyoni
Umeiteka ramani (samaki eh)
Tena uletwe mzani upimwe upendo wangu
Mi ntatoka number one
Ila naimani toka moyoni
Umeiteka ramani
Tena uletwe mzani upimwe upendo wangu
Mi ntatoka number one
Haya

Mi ka samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)
Ntakupa samaki unikubalie, ntakupa samaki (samaki eh)

Nikupeleke visiwani ukale pweza na tasi
(Ntakupa samaki)
Au twende Mwanza ukale sangara na sato
(Ntakupa samaki)
Tupande treni twende Ujiji tupate migebuka
(Ntakupa samaki)
Tumalize Tanga, nyumbani, ukale jodari na ngisi
(Ntakupa samaki)

Nndoto, nndoto, nndoto, nndoto
Nndoto, nndoto, nndoto, nndoto
Samaki eh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI