MISTARI YA WIMBO HUU

Nikiwa kimya sija-mute, nafuga uzima
Lazima nichunge kinywa, sina bima ya sauti
Ulizia shina la maandishi kwa tovuti
Mizizi katika shina, maandishi ya tofauti
Wito sitafuti
Peni bila wino, maandiko matakatifu
Bariki neno kamusi
Asili, asili ni ubinafsi wa akili
Napata njozi Mwokozi akinipa nusu pakuti
Usiniite mkali, mi ni mpole mwenye hasira
Navunja bars kama Paulo na Sila
Taulo ya mpira nikinenepa haiwezi vuka
Nasoma majira, majanga ya Cairo na ajira
Nasikia, mi ndo mwiba
Nachoma mizizi ya mistari, kamari
Navuna pesa za misiba
Napona bila tiba
Na nikikopa kwenye benki ya michano
Narudisha mpaka riba
Twende

Aah Nipe nafasi niwa-show
Ili wanyamaze sio lazima uwakabe koo
Hatu-force kazi kwenye kila ngazi ya flow
Ya kwao haitoki safi na inawapa maprosoo
Mmmxiew Najifanya msoto siuoni
Kwa sababu ndo mtoko wa jioni
Jua likishazama nyota ntaonekana
Mi sio msanii wa soko, sanaa yangu ipo sokoni

Vunja vunja kila rapper…
Teka peni kama hustler
Hatua za baraka kama unyayo wa mufti
Naleta hoja za kujenga, kikao cha mafundi
Kichaa niko fresh, wanaanya
Kitaa na respect ka Jakaya
Vocal nzito kama kwaya
Moon-soon flow, upepo mkali kwenye aya
Moe ndani ya nyumba, flow iko nasty
King nikifika, wapuuzi basi
Na sijiwezi ka snitch anayeropoka
Na dada ‘ako ananiita plasma, na inch za kutosha
Faida za kutosha
Kodi ya maendeleo, maskani natoa ripoti kama bodi ya matokeo
Ona na sumu kama nge, kwahiyo hodi kwa mkeo
Hufanya fake wanafulia, niite dobi wa vimeo

Aah Nipe nafasi niwa-show
Ili wanyamaze sio lazima uwakabe koo
Hatu-force kazi kwenye kila ngazi ya flow
Ya kwao haitoki safi na inawapa maprosoo
Mmmxiew Najifanya msoto siuoni
Kwa sababu ndo mtoko wa jioni
Jua likishazama nyota ntaonekana
Mi sio msanii wa soko, sanaa yangu ipo sokoni

Tuki-tuki, tukitoa utani
Sitokuboa nadhani
Songa ni mwanaume wa shoka, haukumbuki
Kwahiyo shoo zote za bure ye huwa anatoa chumbani
Yaani, ma-rapper wabovu wana chuki nami
Machizi wanauliza nikioa ntatinga suti gani
Haijulikani sifuri gani na nuksi
Mademu wachafu na wanuksi ndo huanika chupi ndani
Mmh Mkuki ndani hauvuki
Chuki amani hautupi
Mtawala ukifa utazikwa na upinzani
Japo tupo kwenye divas’ night
Put your hands up, kama unamuaga Jesus Christ
Ogopa kutukanwa, hakuna dokta wa laana
Wanauliza mbona sijaoa, nafoka kwa sana
Nawajibu nasubiri mke alioachika
Kwa kuwa mke mwema huwa anatoka kwa bwana

Mmh mxshew Nipe nafasi niwa-show
Ili wanyamaze sio lazima uwakabe koo
Hatu-force kazi kwenye kila ngazi ya flow
Ya kwao haitoki safi na inawapa maprosoo
Mmmxiew Najifanya msoto siuoni
Kwa sababu ndo mtoko wa jioni
Jua likishazama nyota ntaonekana
Mi sio msanii wa soko, sanaa yangu ipo sokoni

(Tongwe Records baby)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI