MISTARI YA WIMBO HUU

Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba)
Sasa iweje unaona mi nafaa
Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba)
Sasa iweje unaona mi nafaa

Kosa langu kosa langu ni lipi baba
Kosa langu kosa langu ni lipi baba
Ulinikana tangu tumboni
Ukamkana hadi mama ‘angu
Nyumbani nyumbani wakamfukuza
Shuleni shuleni wakamfukuza
Wakamuita malaya kwa mimba aliyobeba
Yaani mimi jamani jamani jamani
Miezi tisa ilipoada chini ya mbuyu nikazaliwa
Mifuko ya rambo nikafunikiwa
Ili baridi lisinipige
Kwa presha ya mawazo
Mama ‘angu mama ‘angu mama ‘angu
Akaiaga dunia mama ‘angu
Nalia nalia nalia mimi nalia
Nalia ukiwa wa mama yangu
Nalia mimi nalia niacheni nilie

Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba)
Sasa iweje unaona mi nafaa
Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba)
Sasa iweje unaona mi nafaa

Mpita njia mpita njia akaniokota
Akanilea akanisomesha
Nikamthamini akanithamini
Nikamuita mama akajibu mwanangu
Leo nimekua kanisimulia
Inauma sana unajua
Inakera sana unajua
Eti mtu baba ‘ako yupo
Ila hakujali wala hakupendi
Hana time na wewe
Inauma sana inauma sana
Moyo wangu sijui kama utaweza msamehe
Moyo wangu sijui kama utaweza
Sijui kama nitaweza
Nimejaribu nimeshindwa
Kumsamehe mimi siwezi
Siwezi muhukumu namuachia Mungu Baba
Namuachia Mungu muumba wa vyote

Si ulinizaa wewe (baba) ukanikataa (ukanikataa)
Sasa iweje unaona mi nafaa (leo nafaa)
Si ulinizaa wewe ukanikataa (maisha yameninyookea)
Sasa iweje unaona mi nafaa (wewe baba)
Si ulinizaa wewe ukanikataa (kukusamehe siwezi)
Sasa iweje unaona mi nafaa (leo nafaa)
Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba)
Sasa iweje unaona mi nafaa
(Mambo yameninyookea
Ndio unaona nafaaa baba)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI