MISTARI YA WIMBO HUU

Yarabi nipe moyo wa imani uuh nilivumilie penzi
Ilihali mimi sina amani njoo kiu ya mapenzi
Kuishi bila wewe mi siwezi mmh nimpende mwenye ukweli
Nimpende mwenye mapenzi ya kweli
Mmh anitoe mashakani

Kama ni zawadi ya mapenzi nilikupa
Hukunithamini umeniacha umenitupa
Kama ni zawadi ya mapenzi
Hukunithamini umeniacha umenitupa

Unaniona mi sifai (sifai)
Kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri
Sifai (sifai mimi)
Kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri

Najaribu kuisha bila yako hata nia pia ninayo
Kila siku kwangu vitimbi vitimbi
Mwenzako sitaki ugomvi
Nahitaji mapenzi yanijali lakini we huna habari
Kila mara simu yako inazimwa

Kama ni zawadi za magari nitakupa
Hujanithamini leo kesho utanitupa
Kama ni zawadi za ma-Beamer nitakupa
Hujanithamini leo huto utanitupa

Unaniona mi sifai (sifai)
Kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri
Sifai (sifai mimi)
Kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri

Nachotaka si fahari mpenzi
Unadhani tumeishi bila shari
Ukileta mhogo uwe mchungu
Wa penzi lako huwa hauwi sumu
Huna unachotaka wala baby
Vipi uone mi wa kutakataka mali
Mimi sio wa mali
Heey

Nimengoja hilo Bima
Sijaona hata Benz
Nakuacha ufurahi
Kwangu yote kheri
Nimengoja hilo Bima
Sijaona hata peti
Nakuacha ufurahi kwangu yote kheri

Kutoka kwa AY
Mapenzi yangu nilikupa
Kwenye tabu sikukutosa
Ila yote umeyafuta
You let me down oh my baby
Mapenzi yangu nilikupa
Kwenye tabu sikukutosa
Ila sasa umetupa
You let me down oh my baby
Ulizama ndani ya moyo wangu kabisa
Ukatawala akili ukaiteka
Nikakupa ulichotaka we ukadeka
Sasa basi (doze doze moyo wangu upoze)
Kukupenda kukujali I can’t stop
Rudi kwangu kwani milango iko wazi (wazi)
Utanikumbuka one day
What goes around comes around

Unaniona mi sifai (sifai)
Kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri
Sifai (sifai mimi) kunitenda na mapenzi
Nakuacha ufurahi (furahi baby)
Mmh kwangu zote kheri

Sitaki mimi
Kheri tu kwangu mimi
Siwezi eeh kheri

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU